Home » » DC HAPI AWA MGENI RASMI UFUNGAJI MASHINDANO YA VIKOSI VYA JWTZ BRIGEDI YA MASHARIKI

DC HAPI AWA MGENI RASMI UFUNGAJI MASHINDANO YA VIKOSI VYA JWTZ BRIGEDI YA MASHARIKI

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, April 29, 2016 | 6:54 AM

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo amefunga mashindano ya vikosi mbalimbali vya JWTZ Brigedi ya Mashariki Lugalo jijini Dar es salaam.
Hii ni kufuatia mualiko wa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo yaliypfanyika uwanja wa jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.
Akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Brigedi ya Mashariki (Chui) Brigedia Jenerali S.S. Othman alimueleza mgeni rasmi kuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania limekua na utaratibu wa kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, hivyo mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi hayo.
Akizungumza na Maafisa, askari na washiriki wote, Hapi alisema Tanzania imepata heshima kubwa kutokana na jeshi letu kushiriki mashindano mbalimbali kama Olympic na yale ya Afrika Mashariki. Ushiriki huo hauna budi kuendelezwa, alisema Mh. Hapi.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger