Home » » Rwanda:Ntaganda yuko ubalozi wa Marekani

Rwanda:Ntaganda yuko ubalozi wa Marekani

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, March 18, 2013 | 10:30 PM



Bosco Ntaganda
Muasi Bosco Ntaganda anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inadaiwa amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini Kigali, Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema taarifa walizonazo ni kuwa Kiongozi huyo muasi yuko chini ya ulinzi wa Marekani katika ubalozi wake.
"Tumefahamishwa hii leo (Jumatatu) kuwa Bosco Ntaganda ameingia Rwanda na kujisalimisha katika Ubalozi wa marekani hapa Kigali", amesema Louise Mushikiwabo
Jenerali Ntaganda amekanusha mashitaka yanayomkabili katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC kwamba anahusika na uhalifu wa kivita na ule dhidi ya binadamu.
Hata hivyo Marekani haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hizo za kujisalimisha kwa Jeneral huyo muasi katika ubalozini wake.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger