Home » » WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AWASIMAMISHA MAAFISA 6 WA POLISI...

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AWASIMAMISHA MAAFISA 6 WA POLISI...

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, March 10, 2013 | 10:23 PM

 
Waziri wa mambo ya ndani Emmanue Nchimbi amewasimamisha kazi maafisa sita wa polisi kwa tuhuma mbalimbali.

waliosimamishwa ni Elias Mwita mrakibu Mwandamizi wa polisi aliekuwa mkuu wa Upelezi mkoa wa Mbeya, Jacob Kiango Mrakibu wa polisi aliekuwa msaidizi wa mkuu wa Upelezi mkoa wa Mbeya na Charles Kinyongo, mrakibu msaidizi wa polisi aliekuwa mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mbeya.

Hawa wamesimamishwa kutokana na kufanya udanganyifu katika madawa ya kulevya yaliyoshikwa jijini Mbeya mwaka jana ambao wanatajwa kuyaficha kupeleka kidhibiti cha pakti za chumvi.

Askari wengine walipatikana na makosa ya Kupiga na kuwabambikizia kesi zisizo na Dhamana wananchi kutokana na Rushwa ni Peter Matagi, mrakibu Mwandamizi wa Polisi aliekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa kagera.

Askari mwingine Renatus E Chalamila kamishna mwandamizi wa polisi aliekuwa anasimamia Ajira za jeshi la Polisi ambaye alidai na kujipatia fedha ili kutoa ajira kwa wanaotaka kujionga na jeshi la Polisi.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger