Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya JB Belmont, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ndio wadhamini wakuu ndugu George Kavishe amesema “Ninayo furaha kusema kwamba huu utakuwa mwaka wa 12 wa mbio za Kilimanjaro Marathon kufanyika chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager”, kwa mara nyingine ni fahari kwakilimanjaro Premium Lager kudhamini tukio hili maarufu na lenye msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo Tanzania”.
Kavishe amesema ili kuwahamasisha na kuwapa motisha wanariadha wa Tanzania kuongeza viwango vyao na kutumia muda mfupi kumaliza mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager imetenga shilingi milioni kama bonasi au malipo ya nyongeza kwa wanariadha wa Tanzania watakaovunja rekodi kwenye mashindano hayo.
Post a Comment