Ona Wanachadema wanatapatapa kwa Madhambi yao...!!!
Zitto : Kwenye hili tayari umeshinda
Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na mtindo wa kurushwa kwa shutuma mbali
mbali kutoka kwa viongozi wajuu wa CHADEMA wakitumia majina bandia
kumuelekezea ndugu zitto kabwe.
kwa makusudi kabisa viongozi
hao wakiongozwa na mwenyekiti, katibu mkuu na wakurugenzi kadhaa
wamekuwa wakirusha kila aina ya shutuma humu mtandaoni lakini kwa hofu
kubwa ndio maana wanajificha kwa kutumia akaunti bandia.
jana
na juzi nimepokea sms, emails na simu nyingi sana kuhusu hiki
kinachoitwa ripoti ya siri ya SLAA, MBOWE NA WAGAZA WENGINE dhidi ya
ZITTO zikisema namie nimetajwa humo kuwa ninashirikiana na zitto
kukihujumu CHADEMA,
bahati mbaya sana, hakuna ripoti ama
shutuma zozote anazopelekewa zitto kutoka kwa hawa majamaa ambazo
hazinitaji, na kwentye hii nayo nimeshuhudia nikitajwa mara nyingi
kupokea pesa kutoka kwa zitto kukihujumu chama.
bahati mbaya
zaidi ni kwamba wafadhili wa mkakati huu ''OPERESHENI ONDOA ZITTO KWENYE
HOJA ZENYE MASLAHI YA TAIFA'' wamekosa njia sahihi ya kutumia, wamekuwa
wakiwatumia watu wale wale ambao kwa zaidi ya miaka na miaka tumekuwa
tukikitetea chama kuwa si cha namna hiyo.
kitendo cha MBOWE na
SLAA kuwatumia JOSHUA NASSARY, GODBLESS LEMA, MAMUYA na wengine,
kinauthibitishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba zitto ni
tatizo kwenye CDM, kitendo hiki cha kuwatumia watu wanaolalamikiwa kuwa
wanabebana kimisingi ya ASILI ya wanakotokea kinatuthibitishia
watanzania kwamba CHADEMA ni chama cha watu wa eneo hilo.
lakini wamefeli zaidi kumtumia LEMA kuwa eti ni KAMANDA mwenye uchungu
na CHADEMA kuliko ZITTO, hiki pia ni kielelezo cha upeo mdogo wa
kufikiri kwa watu hawa.
ZITTO ni mjenzi wa NYUMBA inayoitwa
CHADENA, zitto ameshiriki mpaka kuijenga CHADEMA tangu ikiwa nyumba ya
nyasi, mpaka ikawa ya udongo, ikaja ikawa ya tofali za kuchoma na sasa
CHADEMA ni nyumba ya VIGAE,
LEMA ni mpangaji tu kwenye hii
nyumba CHADEMA, hakuna jinsi yoyote mpangaji akawa na uchungu na nyumba
kuliko mwenye nyumba, hakuna na haitaka itokee.
LEMA ni mpita
njia tu kwenye CHADEMA, Kamwe hawezi kuwa na uhalali wa kumsema na
kumtukana mtu aliyekijenga chama kilichomsaidia kumfikisha hapo alipo.
Nani humu jukwaani alikuwa anamfahamu LEMA mwaka 2006, NANI?. nani
alikuwa anafahamu lolote kuhusu lema 2007,2008,2009 mpaka 2010 kabla ya
uchaguzi mkuu?.
nani anayemfahamu lema kipindi hicho kwenye CHADEMA?. LEMA ni TUNDA LA KAZI NZURI YA KISIASA ILIYOFANYWA NA ZITTO KABWE.
wakati zitto anahangaika kushirikiana na viongozi wenzake kuijenga
CHADEMA, LEMA alikuwa ni KIBARAKA wa MZEE AUGUSTINO MREMA wa TLP.
Wakati zitto anaibua hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa kama BUZWAGI
na nyinginezo, LEMA bado alikuwa hata hajui chaguo lake la kisiasa
katika nchi hii, yaani lema hakuwa akijua aende chama gani cha siasa.
wanaokumbuka na wenye akili timamu watakubaliana nami kuwa ni zitto
aliyekwenda Arusha kumnadi mgombea wa TLP wa udiwani wakati wa uchaguzi
wa marudio 2008 huku lema akiwa mpiganaji kibaraka wa augustino mrema wa
TLP.
wanachadema wanafahamu kuwa wakati tunafanya uchaguzi wa
ndani ya chama mwaka 2009 LEMA ndio kwanza alikuwa ana siku 4 za
uanachama wake ndani ya CHADEMA.
LEMA anapita tu njia CHADEMA
kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine, ndio maana
alipita NCCR, ILIPOKUFA AKAKIMBIA, AKAPITA TLP ilipokufa akakimbia na
sasa yupo CHADEMA nayo ikiyumba sidhani kama hataacha kukimbia. LEMA
hana hadhi ya kukubali kutumiwa na kina MBOWE na GENGE lake kumshambulia
ZITTO, hana hiyo moral authority. mpangaji hawezi kuwa na uchungu sawa
na mwenye nyumba,
Leo CHADEMA ikipasuka, leo CHADEMA ikiyumba, ikitetereka atakayeumia ni ZITTO aliyeijenga na si LEMA aliyeidandia.
nasisitiza hapa kuwa Hakuna namna yoyote ile inayoweza kumshusha zitto
kwenye heshima yake aliyojijengea kwa kusambaza uwongo wa namna hii,
hakuna na hitakaa itokee.
Hakuna namna yoyote ile ya kumshusha
zitto kwenye orodha ya wanasiasa bora na makini kwa kuwatumia watu kama
kina lema na nassary ambao wakati wanaomba kura waliomba wakisema
WATUMWE WAENDE BUNGENI WAKAWE KAMA ZITTO.
Again, ni rahisi sana
kumshusha zitto kama kuna lolote baya amelifanya lisilo na maslahi kwa
umma wa watanzania. ni Rahisi sana kumshusha na kumchafua zitto kama
njia anazopita sio sahihi, LAKINI SIO KWA UWONGO WA KIPUUZI NAMNA HII.
pamoja na kukiri kuwa zitto ndiye mwanasiasa ninayemuamini na
anayenivutia kuliko mwanasiasa yoyote Tanzania, na pamoja na ukweli
kwamba zitto sio rafiki kwangu bali ni kaka yangu. lakini sijawahi hata
siku moja kupokea pesa kutoka kwake ama kwa MPESA au kwa TIGO PESA tangu
nimefahamiana nae mpaka leo.
ndio maana ninawapa pole MBOWE na vijakazi wake wanaotunga uwongo wa namna hii bila hata kujifikiria mara mbili mbili.
uchaguzi mkuu wa ndani ya chama unawatia homa kundi la mbowe na wagaza
wenzake, uchaguzi huo unawafanya waweweseke kutwa kucha, mchana usiku.
hakuna sababu ya kuhangaika na zitto, wanachadema wapo na wataamua kwa
yale mliyoyafanya, zitto yeye ameshawaacha mile 2000 kwenye siasa zenye
tija kwa Taifa.
nimelazimika kuandika maneno haya baada ya kuona kuna huu ujinga unaofumbiwa macho na viongozi wa CDM kwa makusudi kabisa.
iliwahi kuandikwa humu mtandsaoni kuwa ''zitto ni maporomoko ya nile,
hayazuiliki kwa kifusi'' amewashinda na anaendelea kuwashinda.
Narudia tena kusema KWENYE HILI TAYARI ZITTO AMESHASHINDA.
1. aliwashinda kwenye uwongo wenu mliokuwa mkiusambaza wa kupokea
rushwa TANESCO lilipobumbuluka wakina mnyika, lissu na nassary wote
waliufyata.
2. aliwashinda mlipounda tume ya kumchunguza kuasisi migogoro ndani ya chama.
3. alishinda kwenye hoja ya buzwagi
4. alishinda kwenye hoja ya kuwatimua mawaziri vilaza kwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu
5. amewashinda kwenye hoja ya kuficha mali nje ya nchi (kama mabilioni
ya uswisi) leo mnatapa tapa kwa kuwa bossi wenu anamiliki mali uarabuni.
naomba niwakumbushe kuwa zitto ndiye mwanasiasa pekee wa upinzania
anayeweza kuilazimisha serikali ikafanya maamuzi kutokana na hoja yake
hata kama haipendi kufanya hivyo kwa wakati huo. mfano ni hiyo hapo juu.
naomba nihitimishe kwa kusema, ni kweli kwamba uwongo unapanda ghorofa
kwa kutumia klifti, lakini hauwezi kubadilisha ukweli wa mambo daima
dumu. uwongo utabaki kuwa uwongo tu na utaendelea kupuuzwa milele na
milele.
ndimi.
Habibu mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com
Post a Comment