Mh, Kigwangalla amekuwa akifanya kazi zake kwa ukaribu sana na wananchi wake na hasa wale wananchi wa kawaida. lakini pia amekuwa mchapa kazi Hodari kwa kupambana uku na uku ilimladi mambo yaende sawa Nchini kwetu.
Kwa sasa yuko Uingereza na amesema hivi........!!!
"Nipo
ziara ya kikazi na Kamati yangu nchini Uingereza. Leo mchana saa nane
tutakuwa na kikao cha pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Local Government
ya Bunge la Uingereza (House of Commons), Mhe. Clive Betts, MP akiwa na
wajumbe wa Kamati yake. Tutajifunza kutoka kwao ni namna gani wanafanya
kazi ya kuwa jicho la wananchi kwenye kuisimamia na kuishauri serikali
juu ya kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo ya serikali za mitaa
kwenye nchi yao.'
Lakini pia Hukubali na kuheshimu mawazo na Michango ya wadau mbali mbali, Alisema hivi jioni ya Leo...!!
"Uwakilishi
na uongozi si kazi rahisi sana, siyo kazi ya ukosi mweupe (white collar
job). Ni kazi ngumu inayohitaji muda, uvumilivu na ubunifu wa hali ya
juu. Ni kazi inayotaka mtu ujitoe na uwe tayari kuwahudumia na
kuwatumikia wengine. Kila mtu anakutarajia uwe perfect na wote wanasahau
kabisa kwamba na wewe ni binadamu kama wao tu, na wanasahau zaidi kuwa
kiongozi anatokana na wao. Maisha yangu yote
nimekuwa mpambanaji sana na siku zote sikuwahi kukata tamaa na wala
kukubali kushindwa. Naendelea kuwaomba wananzega wenzangu mzidi
kunisapoti na kunipa ushauri mzuri wa namna bora zaidi ya kuwaongoza
kufikia ndoto zetu za jimbo, wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla. Kuwa
Mbunge siyo kwamba najua kila kitu. Kuwa msomi siyo kwamba sihitaji
elimu. Nahitaji msaada na ninawashukuru watu mbalimbali walioendelea
kunisaidia kufanya kazi hii mf. Ndg. Majaliwa Bilali, Ndg. Furaha Titus, Ndg. Godson Kabamba, Ndg. Gisberth Kabamba, Ndg. Eliphace Fredrick Ruangisa, Ndg. Peter Dafi na Ndg. Kajoro Vyohoroka.
Msichoke kuendelea kuniunga mkono, muda wangu unakimbia kwa kasi ya
ajabu na ahadi kwa wananchi zinahitaji kukamilishwa ili kesho Chama
changu kisipate wakati mgumu wa kujibu maswali magumu mbele ya umma."
Post a Comment