Home » » Mgomo wa wauza Maduka Kariakoo waendelea na Wizi pia Ukiwemo...!!

Mgomo wa wauza Maduka Kariakoo waendelea na Wizi pia Ukiwemo...!!

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, November 19, 2013 | 7:11 AM

 Wamiriki wa Maduka haya wamekuwa hawakai kabisa maeneo haya ya maduka yao, wakifika asubuhi wanatizama Maduka yao kisha kupotea maeneo hayo.
 Nilizungumza na Kiongozi wa POLICE JAMII akasema leo hii palikuwa na vurugu kubwa sana kwani Baadhi ya wamiliki wa Maduka walitaka kufungua lakini Baadhi ya Kundi la wanaosemekana niwamiliki wa Maduka mengine pia waliwazuia wasifungue Maduka yao.
 Kuna waliofungua na Kuibiwa Pia kwani Kuna Kundi la watu wanajifanya wanauchungu sana kumbe lengo lao ni Kuiba Bidhaa za Maduka hayo, Hivo kupelekea watu wengine Kufunga bila hata kuwa na Nia ya Kufunga.
 Lakini Pia kuna walio na Mashine Hizo katika Maduka yao wamelazimika Kufunga pia kwani wakifungua wanakuja wahuni na kuiba vitu vyao na kuwashindikiza wafunge pia ili kuunga Mkono wasio na Mashine hizo.
 Watanzania wengi na wageni toka Nchi za Jiran i wamekuwa wakipigwa na Butwaa wakifika Kariakoo kwani hali ni Tofauti si kama zamani.


 Machinga wadogo wadogo ndo wanafanya Biashara uko Kariakoo Tangu Jana,
 Tangu jana asubuhi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam wafanyabiashara ambao ni wamiliki wa maduka katika eneo la Kariakoo wamefanya mgomo wakutofungua maduka yao kupinga uamuzi wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA wa kutaka kila duka liwe na mashine.
 Madai ya Wafanya Biashara hao ni Kuhusu mashine za Kieletroniki (EFD), Wanalalamika Kuwa wanalazimishwa Kununa Mashine hizo kwa Kuanzia Laki Sita 600,000/= Hadi Laki Nane 800,000/= wanasema Kiwango hiko ni kikubwa sana hawawezi kununua.
Lakini pia wanadai kuwa hawashirikishwi krk Vikao vya Maamuzi.
 Bango hili linasomeka hivi "HATUTAKI MASHINE ZA T.R.A" sasa Mi naomba Mtanzania wewe Utafakari Kugomea Kulipa Kodi ni sahihi au laa...!!!?
Nani alaumiwe apa Mlipa kodi aliegoma, TRA, Serikali au Nani haswa?
  Maduka yote yaliyopo Kariakoo Mtaa wa Msimbazai, Uhuru,Lumumba, Aggrey,Mchikichi,Narung’ombe,Tandamti, Congo na meneo mengine kote maduka yalifungwa baada ya kutangaziwa hivyo na umoja wa wafanyabiashara.
 Katika Tamko au Majibu ya Serikali jana Naibu waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum,  Alisema Wizara ilikaa na wasambazaji wa mashine Hizo na Kukubaliana kuwa Mashine hizo ziuzwe kwa Kulingana na Hadhi yake na sio kila mashine iuzwe laki Nane, (800,000) Lakini Pia Mkuya alisema kuwa Serikali haina nia ya Kuwakomoa wafanya Biashara hivo lengo ni Kukusanya Kodi kwa wafanya Biashara wote ili serikali ipate Fedha za Kufanya Maendeleo ktk Nchi Nzima. Hivo kasema Swala Hilo Litafanyiwa Kazi .
Lakini Alitoa Mapendekezo kuwa Wafanya Biashara wajiunge kwenye vikundi ili wapewe Mashine Hizo kwa Mkopo na walipe baadae, Lengo ni kuwasaidia tu Watanzania kukua Mashine Hizo.
 Mtaa wa Kongo Kimyaaa hakuna shamla shamla za vurugu kama ilivyozoeleka.
 Hapa ni Maeneo ya Kuingia Kariakoo Shimoni Kote Huku kumefungwa Maduka yote.
 Nilipata Fulsa ya Kuzungumza na Kiongoji wa POLICE JAMII wanaofanya ulinzi mitaa ya Kariakoo.
Akikuwa na Haya yakusema, Kuwa wao kama Police Jamii kwa siku mbili hizi wamekuwa na changamoto kubwa zaidi kwani vibaka wamekuwa wengi sana, Pamekuwa na Kundi la wahuni wakiwadanganya watu wanaoenda kununua vitu Huko Kariakoo.
NOTE:-
WAFANYA BIASHARA NI LAZIMA WALIPE KODI YA MAUZO(VAT) SERIKALI ISIYO KUSANYA KODI HAFAI KUWAKO MADARAKANI TRA ITAFUTE NJIA MBADALA YA KUWAUZIA MASHINE WAFANYA BIASHARA HAO,NCHI ZILIZO ENDELEA TUNALIPIA MACHINE HIZO KWA MWEZI KWA KWA MKATABA WA MUDA FULANI 1yrs+ HII INAWEZEKANA KUWEKO NA RIBA KIDOGO,WAFANYA BISHARA WATU WANA PASWA KUELIMISHWA KWAMBA WALIKUWA WANAFANYA BIASHARA BILA KULIPA KODI NI KINYUME NA SHERIA TENA WANA PASWA KUTOZWA FAINI AU KULIPA MALIMBIKIZO NAJUA WANASIASA WATALI RUKIA KISIASA WAFANYA BIASHARA WASIOTAKA KULIPA KODI WAFUNGIWE LESENI ZAO NA MAENEO WAPEWE WATU WENGINE WALIOKUWA TAYARI KULIPA KODI
Hakika watanzania tumekuwa na Kasumba mbaya sana yakugomea Kila kila kitu kinapotakiwa kufanyika kwa Lengo la Kusaidia serikali na baadae kutusaidia Watanzania kwa Ujumla, Swala la Kodi hawa wanaogomea lao wamekuwa sin walipa Kodi kwa Muda sasa lakiki hawaoni Aibu yakutokufanya hayo na bado wanataka kutokuendelea kulipa, Jamani tufahamu Kodi zetu ndio mafanikio yetu, Tulipe Kodi na tuisaidie serikali yetu.
Lakini Kubwa zaidi TUIPENDE TANZANIA YETU KWAKUJADILI MEMA NA MAZURI YA NCHIN YETU KWA FAIDA YETU NA KIZAZI CHETU KIJACHO.
Mungu IbarikiTanzania.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger