Jana ni siku ya furaha sana kwa Mrs Lucas
Zuria au unaweza kumwita mama King Stone au wengi wanamwita Pipi jina
ambalo alianzia nalo mziki wakati akiwa pale THT. Usiku huu mungu
amemjalia amejifungua salama mtoto wa kiume na kuongeza familia yenye
watoto wawili wa kiume. Katika account yake ya Instagram na Facebook
ameandika status nzuri huku akimwonyesha mtoto huyo mpya kama umwonavyo
kwenye picha.
“Nina furaha mpaka sijui nisemeje
maana naweza nikaandika essay hapa lakini kwa ufupi tu…namshukuru mungu
kwa kunipa nguvu…uhai…na mume wangu kipenzi kwa kunipa ujasiri wa kuleta
jembe la pili…Asset kubwa kuliko zote duniani asikwambie mtu!!! Welcome
to the family baby Brandon !!! #babynumber2″
Post a Comment