KUNA TISHIO LA CCM WILAYA YA NZEGA DHIDI YA DK. KIGWANGALLA KUTOKANA NA MASWALA YALIYOTOKANA KATIKA BARAZA LA MADIWANI.
Mizengwe na Fitna ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa sasa si jambo geni wala Habari ya Kustua. Pengine hiyo inaweza kuwa kuwa ni ushaidi wa baadhi ya viongozi WAZALENDO wanaopiga Vita makundi ndani ya Chama hivo kujikuta wanaandamwa na wenzao kila Kukicha.
Mamoja na mengine Moja kati ya Matatizo Matatu ndani ya Chama hicho ni Mdudu Rushwa aliyeshika Mizizi kutengeneza kundi la wanachama wachache wenye Fedha wanaothaminiwa na Kutukuzwa, Huku wenzano wazalendo wakiwekwa Kando na kubezwa kwa juhudi zao.
Mifano ya Hali hii iko mingi sana, Lakini moja wapo ni sakata lililosababisha uamuzi wa CCM Wilaya ya Nzega , wakutaka kumvua uanachama Mbunge wa Nzega Dk, Hamisi Kigwangalla chanzo kikiwa ni kusimamia vizuri Fedha za Halmashauri
Sakata hilo linatokana na Madai ya kuwatusi Viongozi ndani ya Jimbo hilobaada ya kutofautiana Kimtizamo katika Matumizi ya Sh 2.3 Billioni zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji wa madini Resolute kama kodi ya Huduma kwa Halmashauri hiyo.
Dk, Kigwangalla pamoja na madiwani kadhaa wanapinga kupindishwa kwa Adhimio la Baraza la Madiwani amablo lilielekeza Fedha hizo zitumike kuanzisha Benki ya Jamii ya Nzega (Nzega Community Bank Ltd-NCB) na Kampuni ya Ujenzi ya Jamii ya Nzega (Nzega Community Construction Corporation Ltd - NCCCL) Huku wakibadili mawazo wakitaka zipelekwe katika Kata, Ambapo inaaminika zingeweza kutumika Vibaya.
Kutokana na mazingira hayo Tulifanya mahijiano na Mbunge wa Nzega ili kujua hatima yake endapo chama kikiamua kumvua uanachama......
Swali:- Viongozi wako wa wilaya wametishia kukuvua uanachama, umechukuliaje hali hiyo na unampango gani iwapo hatua hiyo ikitekelezwa?
Jibu:- Sini chama changu kikinivua uanachama. Hao wanaopendekeza ivo ni watu wadogo sanakwenye chama wanaojikuta kutafuta umaarufu wa burebure.
Pia mimi sikuingia CCM kutafuta Cheo Ninatokana na CCM, Nimelelewa na CCM, na sioni tatizo hawa wavamizi wachache wakinitoa kwenye mstari.
Najichukulia kama hazina ya uongozi wa CCM na sioni kwanini nitetereke hata nifikie nianze kutafakari kuhamia chama kingine.
Ninaamini kwenye CCM imara kwenye kuandaa viongozi thabiti wa kesho kwa ustawi wa Tanzania.
Swali:- Unadhani tuhuma hizo ndizo chanzo pekee cha wewe kufikia hatua ya wewe kutaka kuvuliwa uanachama?
Jibu:- Kwanza niweke wazi hakuna tuhuma yoyote ile kwa mimi kufananisha madiwani na Mizigo Maana nimewafananisha tu.... Si kweli kuwa wao ni Mizigo. Hata kama kumfananisha kiongozi mbovu na mchumia tumbo na mzigo si sawa, basi wakwanza kutuhumiwa na kufukuzwa chama angekuwa ni Abdulrahmani Kinana katibu mkuu CCM, Maana yeye ndie ameuhasisi huu Msamiati wa "Mizigo" .
Tatizo kubwa lilipo hapa ni huu Ubunge wangu... Kuna mtu mmoja mpumbavu anadhani atanyakua kiti hiki kwakunifukuza katika Chama.
Hii si mara ya kwanza niya Tatu. Nimeshazoea sasa hali hii, na ninahakika hata chama sasa Makao Makuu wanalijua hili na ndio maana wamekuwa wakipuuzia tu.
Binafsi sina tatizo sana na kukosa Ubunge. Hii ni kazi ya utumishi wa Umma nani ngumu sana kuliko watu wengine wanavyodhania. Labda uwe Mbunge "Mzigo" Usieifanya ipasavyo kazi hii.
Mimi ninajituma sana kutekeleza majukumu yangu na wananchi wananiunga mkono, Hiyo ndio nguzo yangu kuu.
Kuna watu wanawasiwasi sana kwa jinsi ninavyozidi kupendwa na kuungwa mkono na wananchi wa Nzega, sasa wanaweweseka na kutafuta njia za kunichafua ndani ya chama ili nionekane Tatizo.
Wanauwinda Ubunge wangu kama Fisi anavyowinda Mkono wa mwenda kwa Mguu. Wapeni Taarifa tu kwamba Sikuingia kirahisi na kutoka kwangu itakuwa Mbinde...!!
Kinachonipa moyo nikwamba wananchi wapo pamoja na mimi, Pia chama hiki waga hakikurupuki, Kinamfumo wakukusanya Taarifa Hivyo ukweli utathibitika na Haki itatendeka.
Swali:- Pamoja na mazingira hayo, Hali ya ushindani ndani ya chama katika kugombea Jimbo lako Ukoje?
Jibu:- Sioni ushindani wowote ule wakutisha jimbini kwangu, Sema kuna watu waliokata tamaa na ndoto zao za kisiasa.
Wangekuwa makini wangejiuliza waliteleza wapi wangejilekebisha. Nasema sina upinzani kwa sababu kazi yangu inajionyesha, sidhani kama wananzega watakuwa tayali kubadilisha Almasi kwa Jiwe.
Kazi yangu imeonekana na inajieleza yenyewe, ya hao wanaoangaika hakuna hata mmoja aliyeiona, Sasa kama nitaamua kugombea tena Ubunge sidhani kama wananzega watajiuliza mara mbili mbili kudhihirisha hilo. Kuna siku moja niliwahi kutamka kuwa nimechoka fitna na Majungu ya Nzega yanayopikwa na wenzangu katika Chama, hivyo ninaweza nisigombeee......
Wazee waliniita wakaniweka chini wakanambia 'Koma' na usiseme tena hayo maneno! Vijana wakasema ninani anayekusumbua tumshughulikie .....! Hii ni sapoti kubwa sana na naiheshimu na siwezi kuwabeza watu hawa kwakuwa wamenipa heshima kubwa sana.
Swali:- Je..! Unadhani msimamo wako huu ndani ya Chama hautaadhiri uanachama wako?
Jibu:- Ninaamini hautaathi kwa sababu waliofanya uamuzi huo wana upofu wa ukweli na hawajui kanuni na taratibu za chama na hata msingi tu ya haki ya Binadamu.
Huwezi kutoa hukumu ya haki hali yakuwa uanamaslahi yako binafsi kwenye jambo unalolisikiliza, na pili kimsingi huwezi kuwa mhudumu alafu ukang'ang'ania uhakimu, Huwezi kufikia hatua ya kutoa hukumu bila kuwasikiliza watu.
Nimalizie kwa kusema kuwa CCM sio kikundi cha wahuni, ni chama cha Siasa chenye utaratibu makini wa kukiendesha na kwakuwa mimi ninaelewa taratibu za chama, Kanuni na Sheria. Sioni uamuzi wa hawa wachumia Tumbo ukisikilizwa na kuzingatiwa na chama na kama vikao vya juu vya chama na kama vikao vya juu vya chama vitaamua kuwasikiliza basi msimamo wangu uko wazi, tutakuwa tumepotea kama mimi binafsi sitaona haja ya kuwa ndani ya chama.
Hapo hata kama nikifukuzwa uanachama ndani ya chama sinto - regret chochote (Sitajutia) maana chama kitakuwa kimetoka kwenye misungi.
Post a Comment