Kukataliwa kwa ripoti hiyo kumempa wakati mgumu
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, ambaye amehamishiwa jijini
hapa hivi karibuni.
Chini ya uenyekiti wa Dk Hamis Kigwangalla, kamati
hiyo ya bunge licha ya kubaini matumizi mabaya ya fedha za miradi
iliyokusudiwa, pia ilibaini kutokuwepo kwa umakini katika utendaji wa
kazi wa maofisa wa Jiji la Mwanza, ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini.
Kutokana na mkanganyiko huo, Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Dk Kigwangalla alidai kuwa ripoti iliyotayarishwa kwa mara ya pili
kama ilivyokuwa ya awali, haieleweki.
Akizungumza katika ukumbi wa halmashauri hiyo
jana, Dk Kigwangalla alisema majibu yaliyotolewa baada ya taarifa ya
awali kuhusu miradi mbalimmbali ya maendeleo, si ya kweli na kwamba
yanaipotosha kamati.
Aliwataka watendaji kuandaa nyaraka zote za miradi ukiwemo ule wa ujenzi wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Mwanza.
“Kamati imesikitishwa sana na namna ya uandaaji wa
taarifa ya halmashauri ya jiji hili, hii ni pesa ya umma inakuwaje mtu
unakosea kujumlisha hesabu na kutoa takwimu ambazo si sahihi kabisa,”
alihoji Dk Kigwangalla.
Post a Comment