Home » , » Madai ya Serikali kufilisika na yanayoendelea ndani ya Wizara ya Fedha!

Madai ya Serikali kufilisika na yanayoendelea ndani ya Wizara ya Fedha!

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, February 4, 2014 | 6:36 AM

Wakuu,

Wakati Serikali ikidaiwa kushindwa kuwalipa watumishi wake mshahara wa mwezi Januari 2014 mpaka sasa, kuna tetesi kuwa Waziri wa Fedha aliyeteuliwa na Mhe. Rais hivi karibuni Mhe. Saada Mkuya amewaandalia wajumbe wote wa Kamati ya Bajeti ya Bunge pamoja na maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha safari ya kufanya 'utalii' kwenye nchi za Sweden ama Norway kwa muda wa siku zaidi ya kumi kama njia ya kujipongeza na kuwaweka sawa wabunge hao kwa bajeti atakayoiwasilisha katikati ya mwaka huu. Safari hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 02 - 12 Februari, 2014.

Safari hiyo iliyobatizwa 'Study Tour' kwa ajili ya kujenga uwezo kwenye mambo ya bajeti na ukusanyaji wa mapato itajumuisha ujumbe wa watu zaidi ya thelathini ambao watagharamiwa kila kitu na Wizara ya Fedha ama Hazina jambo linaloonekana kuwa ni staili nyingine ya kutoa takrima kwa wabunge ili wapitishe bajeti za wizara husika bila mikingamo mingi baada ya staili aliyotumia aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo Bw. Jairo kugundulika hali iliyosabisha kupoteza nafasi yake.

Jambo la kujiuliza ni kuwa; inakuwaje Serikali inalalama kila siku kuwa haina fedha jambo linalopelekea kushindwa kulipa hata mishahara ya watumishi wake kwa wakati lakini inakuwa na uwezo wa kugharamia safari zisizokuwa na tija kwa taifa na ambazo zinagharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi?

(Nusanusa yetu imepata viambatanishi kadhaa kama uthibitisho wa kinachojiri ndani ya Wizara ya Fedha katika suala hilo ikiwemo barua na orodha ya wanaotakiwa kusafiri pasipo kujumuisha maofisa wengine ambao wako kwenye level ya chini)












CHANZO:- Jamii Forum
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger