"Tarehe 6/3/2014 siku ya Alhamisi baadhi ya wenyeviti wa uvccm wilaya walikutana Dodoma nakujadili agenda zifuatazo 1.kuunda dhumuni la uanzishwaji wa umoja 2.muundo wa uongozi na uteuzi wa viongozi 3.kupanga tarehe ya kukutana rasmi wenyeviti wote wa wilaya nchi nzima.Agenda iliyopewa kipaombele ilikuwa agenda namba mbili ambayo ilipelekea kupata viongozi walioitwa wampito kama ifuatavyo;mwenyekiti wa wenyeviti wa wilaya nchi nzima ni Ndg.Sango Kasera(Rorya),makamu mwenyekiti Bara Ndg.Malanyingi Matukuta(Mbeya mjini),Katibu mtendaji Ndg.Shaban Bwanga(Dodoma mjini) akisaidiana na Ramadhani Bendera(Korogwe vijijini),Visiwani hakuna mwakilishi,walioteuliwa kuwa makatibu wa kanda ni Japhari(Mwanga)-Mash,Bendera(K
Napenda sana kushirikiana na wenzangu,kujumuika nanyi na kusaidiana kwa kila hali nilithamini mawazo yangu na ya watu wengine kwa faidi ya wenzangu na chama changu,ila kwa sasa nimeamua kwa ridhaa yangu kujitoa katika mchakato huu wa uanzishwaji wa umoja wa wenyeviti wa wilaya wa uvccm si kwa utashi wa mtu nikwa mapenzi yangu na kwa faida ya vijana makini Tanzania nikiendelea kuamini kuwa bila umakini umoja huu hautoweza kufanikiwa.Lazima tuzingatie maslahi ya wengi kuliko maslahi binafsi.
Baada ya kupata taarifa hizi nimeamua kung'atuka nafasi ya uongozi niliyopewa kwenye umoja huo ili kulinda heshima yangu kwa kuwa mchakato huu ulikuwa wa vyeo si dhumuni. Pia kuunga umoja ndani ya umoja bila kupata idhini ni jambo ambalo linakiuka taratibu za chama. Siko tayari kuwa miongoni mwao.
Ahsante naomba kuwasilisha,
By JK.Mghamba-M/Kiti Uvccm Mwanga.
Post a Comment