Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la Uchumi
la Dunia kwa Bara la Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa viongozi
wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani Afrika waliotunukiwa tuzo ya kuwa
viogozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.
Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo
ya Makazi, aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika
masuala ya siasa barani Afrika kwa mwaka 2012.
Kwa mujibu wa kampuni ya Microsoft kutoa Marekani inayojihusisha na
masuala ya Kompyuta iliyoandaa tuzo hizo, Mdee na Kanza ni miongoni mwa
viongozi jasiri katika masula ya siasa kutoka barami Afrika ambao
wanahitaji kupongezwa.
“Mwaka 2012 ulikuwa mwaka mzuri kwa viongozi wanawake wa kisiasa pamoja
na marais wawili wanawake na viongozi wawili wanawake kutoka Umoja wa
Afrika, Microsofti iliangalia wanawake 11 ambao wako makini katika
masuala ya siasa barani Afrika,” ilieleza sehemu ya maelezo yaliyowekwa
kwenye mtandao.
Wengine waliotunukiwa ni Rais wa Malawi, Joyce Banda; Rais wa Liberia,
Ellen Johnson Sirleaf; Mbunge kutoka Kenya, Charity Ngilu; Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Louise Mushikiwabo
na Waziri wake wa Afya, Agnes Binagwaho.
Wengine ni Rais wa Muungano wa Afrika, Nkosa Zana Dlamini Zuma; Waziri
wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okojo-Iweala; Makamu wa Rais wa Zimbabwe,
Joyce Mujuru na Mwenyekiti wa chama cha CPPG cha Ghana, Samia Nkhrumah.
Post a Comment