Home » » MAMA AUWAWA BILA HATIA YOYOTE

MAMA AUWAWA BILA HATIA YOYOTE

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, May 26, 2014 | 2:06 AM

INASIKITISHA SANA HII...

TUMCHE MUNGU ILI TUWE NA HEKIMA BUSARA NA HEKIMA ZA MUNGU PIA ILE HOFU YA MUNGU


Maisha ni kitendawili kigumu sana kukitegua japo wapo wanafanikiwa kukitegua kwa urahisi na kufanikiwa katika maisha . Mama huyu alikuwa na watoto watatu mmoja akiwa anasoma shule ya msingi darasa la tano na mwingine darasa la pili huku akiwa na mtoto mdogo kabisa wa miaka mitatu kwa bahati mbaya kila mtoto alikuwa na baba yake

Matatizo yakamuandama mama huyu kwani mtoto wake wa darasa la tatu alifukuzwa shule kisa kutokuwa na pesa za michango pamoja na ada huku mtoto wa darasa la pili alikuwa anaumwa sana na yule mtoto mdogo alikuwa kalazwa katika hospitali kwa matibabu ya kiribatumbo

Manesi hawakuisha kumtukana kutokana na mama huyu kutokuwa hata na pesa ya kutoa rushwa hospitalini hapo .Alitegemea chakula kutoka kwa wagonjwa wengine wale wabakize kisha na y eye ampatie mtoto wake anaeumwa
Baada ya siku kadhaa kukaa hosipitalini aliruhusiwa kurudi nyumbani kufika nyumbani akakuta Yule mtoto aliemuacha anaumwa kazidiwa huku ndani hakuna hata chakula na Yule mtoto mwingine analia njaaa na ndani hakuna chakula

Kutokana na hali maisha yake kuwa magumu basi mama huyu akawa mchafu na watu wa pale wakamtuhumu kuwa ni mchawi alimpeleka mtoto wake hospitalini mtoto alilazwa manesi walimwambia aende akalete chakula akaondoka hospitalini akiwa kamuacha mwanae kalazwa wakati yupo njiani basi akaona mazao kwakuwa nyumbania alijua hakuna chakula hivyo akaona bora aingie katika shamba hilo achukue mazao kidogo ili akampikie mwanae chakula

Bahati mbaya sasa wakati yupo kwenye shamba vijana wakatokea na kumtuhumu anawanga katika shamba hilo kwani mavazi yake yalimuacha wazi maeneo mengi ya mwili wake na yeye alipowaona aliinama ili wapite vijana hao walimshambulia kwa kumpiga kasha kumchoma moto mpaka umauti ukampata pale pale 







SI VYEMA KUCHUKUA HATUA MKONONI KWA JAMBO LOLOTE LILE.

Share na wenzio waone comment chochote hapa ukimuombea mama huyu
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger