Home » , » Aliyekuwa waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba Apunguza Shahidi Mmoja katika Kesi yake

Aliyekuwa waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba Apunguza Shahidi Mmoja katika Kesi yake

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, June 18, 2014 | 3:16 AM


WAZIRI wa Fedha wa zamani, Basil Mramba anayekabiliwa na ke ya matumizi mabaya ya madaraka na kusabaisha hasara ya Sh,bilioni 11.7, jana aliambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, anamuondia shahidi wake wa tatu ambaye  alikuwa ni  Naibu Kamishna wa Income Tax , Felisian Busigala  katika orodha ya mashahidi ambao awali alikuwa anataka amtetee.

Kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya jopo la majaji wa tatu, John Utamwa, Sam Rumanyika na  Sauli Kinemela kuja kutoa uamuzi pingamizi lililowasilishwa na upande wa jamhuri ambalo liliomba mahakama hiyo, imuondoe Busilaga katika orodha ya mashahidi wa Mramba  kwasababu  hastahili kuwa shahidi katika kesi hiyo kwasababu ushahidi alioanza kuutka Septemba 20 Mwaka 2013 anaonyesha amefika mahakamani hapo kama mtaalamu wa masuala ya kodi na siyo shahidi ambaye anastahili kuzungumzia mashitaka yanayomkabili Mramba.

Wakili wa Mramba, aliwasilisha ombi Hilo la kuomba Mahakama imuondoe shahidi wa mRamba Katika orodha ya mashahidi wake, ombi  ambalo lilikubaliwa na Jaji Utamwa , na Wakili Swai aliomba Kesi hiyo Iarishwe hadi Agosti 21 Mwaka huu kwaajili ya kusikilizwa kwasababu Jana, hawakuwa wamekuwa na shahidi, ombi ambalo lilikubaliwa na jopo Hilo.
Septemba 20 mwaka jana,  mawakili wa serikali waandamizi Shadrack Kimaro na Oswald Tibabyekomya mbele ya jopo la majaji watatu John Utamwa ,Sam Rumanyika na Hakimu Mkazi Saul Kinemela ikiwa ni saa chache tu tangu shahidi huyo wa tatu wa Mramba ambaye pia ndiye Kamishna wa kwanza nchini wa  Costumes   Exercise wa TRA ,kupanda kizimbani na kuanza kutoa ushahidi wake huku akiongozwa na wakili wa Mramba, Hurbbet Nyange kutoa ushahidi wake.

Wakili Tibabyekomya aliomba akiwasilisha pingamizi hilo aliomba shahidi huyo asiendelee kutoa ushahidi wake kwasababu ushahidi aliokuwa ameanza kuutoa jana asubuhi unaonyesha Busigala amefika mahakamani hapo kutoa ushahidi wa kitaalamu na siyo kutoa ushahidi unaohusu mashitaka yanayomkabili Mramba  na kwamba mawakili wa upande wa utetezi wamekiuka utaratibu wa kumleta shahidi huyo kwani wamemleta shahidi kama mtaalamu badala ya shahidi.

Baada ya kusikiliza ombi hilo la upande wa jamhuri, Jaji Utamwa alisema shahidi huyo kwa jana hataweza kuendelea kutoa ushahidi wake kwasababu upande wa jamhuri umewasilisha pingamizi hilo, na akautaka upande wa utetezi uwasilishe majibu ya pingamizi hilo Oktoba 14 , upande wa jamhuri ujibu Oktoba 21   na uamuzi wa pingamizi hilo utatolewa Oktoba 25  na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kuanzia tarehe hiyo ya Oktoba 25 hadi 29 mwaka huu, na akamtaka shahidi huyo asije mahakamani hadi pale mahakama hiyo itakapotoa uamuzi wa pingamizi hilo na akasema kesi hiyo itatajwa Oktoba 18 mwaka huu na akapatia kibali cha kusafiri nje ya mkoa washitakiwa wote.

Mapema jana asubuhi Busigala akiwa kizimbani akijibu maswali ya wakili Nyange ambayo yalimtaka shahidi huyo afafanue maana ya ‘Net of all taxes’ kwasababu kwa mujibu wa mkataba ulioingiwa na Benki Kuu na kampuni ya Alex Stewart inaonyesha BoT kwaniaba ya serikali iliridhia kampuni hiyo ichukue asilimia 1.9 ya dhahabu yote atakayokuwa ameishaikagua.Na aieleze mahakama kuwa je  Mramba alikosea au alikuwa sahihi kwa hatua yake ya kutoa msamaa wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart? Na je Waziri wa Fedha anayo mamlaka ya kusamehe kodi kampuni?

Busigala alianza kufafanua kuwa ‘Net of all taxes’ katika mkataba ule maana yake kampuni ya Alex Stewart  ataondoka na asilimia 1.9 baada ya kumaliza ukaguzi wa dhahabu  na hiyo asilimia 1.9 ni baada ya  kodi yote kukatwa na serikali na kwamba kama kisingekuwepo hicho kipengele kwenye ule mkataba ni kwamba kampuni ya Alex Stewart  angelipwa fedha zaidi na serikali ili mwisho wa siku kampuni hiyo iweze kuja kulipa kodi husika kwa serikali na tatizo hapo siku zote kodi zimekuwa zikibadilika badilika kwani zinapanda na kushuka  na hivyo ingelikuwa ni vigumu kwa serikali  kuweza kutekeleza matakwa ya mkataba ambao usingekuwa na kipengele hicho cha kumlipa moja kwa fedha kampuni na kisha kampuni ije ilipe kodi husika kwa serikali.

Maelezo hayo ndiyo yalisababisha mawakili wa upande wa jamhuri kuwasilisha pingamizi hilo ambalo lilisababisha mahakama kumtaka shahidi huyo asindelee kutoa ushahidi wake hadi watakaposikiliza pingamizi hilo kwa njia ya maandishi na watalitolea uamuzi Oktoba 25 mwaka huu.Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa mfululizo rasmi Jumatatu ya wiki hii na kumalizika jana.

Novemba 2008 ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mipango na Uchumi Gray Mgonja wanakabiliwa na makosa mbalimbali ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 11.7.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger