Home » » Majambazi wamuuwa Sister wa Parokia ya Makoka kwa Risasi Ubungo

Majambazi wamuuwa Sister wa Parokia ya Makoka kwa Risasi Ubungo

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, June 23, 2014 | 8:30 AM


SISTA wa Parokia ya Makoka iliyopo Kibangu, Dar ameuawa na majambazi yaliyokuwa kwenye bodoboda wakati akiingia kwenye gari akitokea dukani eneo la River Side, Ubungo jijini Dar es Salaam hivi punde.

Kabla ya kuuawa sista huyo, dereva wake alipigwa risasi mkononi na majambazi hayo.



Alikuwa anapeleka pesa bank alikuwa kwe tax. Walipofika maeneo ya msikitini ndio wakavamiwa na hao watu wawili walikua kwe pikipiki wakapiga risasi kwa nyuma ya gari ikampata sister kwe kichwa na nyingine ikampata Dereva kwe kidole gumba kikachambuka kama mchicha.

Mwili wa mtawa ukiwa umefunikwa.

Risasi nyingine ikapigwa hewani watu wakaanza kukimbia ndo wale majambazi wakaingia ndani ya ile taxi na kuchukua pochi ya sister.


Dereva akionesha kidole gumba kilichopigwa risasi.

Ila walibugi stepu maana pesa hazikua kwe pochi zilikua kwe gari. Mungu ailaze pema roho ya sister na Dereva apone haraka ili arudi kazini salama.
 
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger