Home » , » Paul Makonda amuapisha Steve Nyerere kuwa Kamanda wa CCM Tawi la Bwawani .Picha zaidi hapa...........

Paul Makonda amuapisha Steve Nyerere kuwa Kamanda wa CCM Tawi la Bwawani .Picha zaidi hapa...........

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, June 27, 2014 | 10:56 PM

Msanii JB akizungumza na wananchi kisha kutambulisha jopo la wananii walokuja kumsaport mwenzao Steve Nyerere

Hapa ni kundi la wasanii wa Bongo Movie

Wasaniii Maarufu walikuwepo

Nyomiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Mwenyekiti kata ya Bwawani CCM akimkalibisha  Mgeni Rasmi kuja Kuhutubia wananchi na kishs Kumsimika Ukamanda Steve Nyerere

Hapa ni Paul Makonda alielekea Jukwaani kuhutubia Umati wa wanachi wa Bwawani Mwananyamala

 1. Alisema Ukamanda ni kazi kubwa sana anapewa Mtu, Kwani kazi yake kubwa ni  kupigana kuhakikisha Chama kinasimama Imala ivo Steve Nyerere ahakikishe Chama cha Mapinduzi kinasimama imara Bwawani na kuleta Wanachama wengi zaidi.

2. Alizungumza uongo wa CHADEMA na vyama vingine na umoja wa UKAWA ni kudanganya watu na kusemea unafiki na chuki ili wachukie Nchi, alisema Tizama Wanatafuna Luzuku kwa Kula na Kujenga pia ku nunua Magari nk.... Hii wameshindwa hata kujenga Ofisi zao CDM.
CDM ni Kampuni kwani kila kitu kinajina la Mtu pale sio Mali ya Taasisi mfano ni Zile Gari za Movement for Changes, hawa wanafanya Biashara kwa Watanzania, hivo Tuwakatae.

3.Katiba Mpya ambayo iko katika Rasimu na ilikuwa inajadiliwa Bungeni Dodoma, Katiba Mpya hii ilidaiwa na Wanasiasa wakaichukulia hiyo kama Utatuzi wa Matatizo yao wanasiasa kwa Maana ya kupata Vyeo ktk Katiba hiyo, hii ni UKAWA walotoka Bungeni wanataka kudanganya watu kuwa eti Katiba itabadili Maisha ya Watanzania kitu aambacho si kweli.

Serikali tatu si Mbadala wa kutatua Matatizo ila chanzo cha kuzidisha matatizo nchini hasa kwa wananchi kwani garama zitaongezeka za maisha kwa kuendesha Serikali mpya ya tatu..

UKAWA wamepata wafadhili nchi za nje na wanalipwa Laki Nne na nusu kila wanapotoka Bungeni na kuendesha Mikutano nje ya Bunge, Taasisi hiiinawafadhili toka ulaya ili tusiwe na amani Nchini ili wao waje kuchukua Rasilimali zetu .

alisema Paul Makonda

watu teleeeeeeeee

Baada ya Hotuba Makonda alimuita Steve Nyerere na Kuanza zoezi zima la Kumsimika Ukamanda

Alivalishwa Vazi MAALUM LA KIKAMANDA, Mkuki kwa ishara ya siraha ya kupigana na maadui waovu, pia Ngao ikiwa ishara ya Kinga kwa makombola ya Maadui

FUraha ilitawala baada ya Kusimikwa

Alipokea zawadi toka kwa Ndugu, Jamaa na Makada wa chama, hapa ni Mama yake Mzazi akimvisha Kaka Mama yake pia ni Kiongozi wa chama mtaani hapa

Mama yake Steve Nyrere akimvisha Kanga, Mama ni Katibu wa Chama mtaa wa Bwawani

Mwenyekiti wa CCM Bwawani , akiwa na Mgeni rasmi wakimvisha Beji Nyerere

Baaada ya Kusimikwa ukamanda alipanda jukwaani na kuhutubia wanachi

Tema checheeeeeeeeee
 Kamanda wa Chama cha Mapinduzi Bwawani alisema kuwa Alizaliwa ktk Familia Duni sana lakini amekuwa mpiganaji sana mpaka hata anaona mafanikio kupitia Jitihada zake, Hivo basi anawaahidi WanaCCM kuwa atahakikisha ushindi wa chama cha mapinduzi kuanzia kata hadi mkoa.
Kamanda akibariki uma kwa maneno makali ya Kikamanda

Dada huyu ni mwanamitindo alikuwa Marekani kwa Muda Mrefu akifanya Mitindo Dada Asia Idarosi alikuja pia

Meza kuu wakiteta kidigo

Hawa ni Wasanii wa Bongo Flaver wakifaamika kwa jina la Makomando wakitumbuiza ktk Tukio hilo la Usimikwaji wa Ukamanda.

William Malecela alizungumza na wanachi baada ya kukaribishwa na Wasanii wa Bongo Flaver kusema neno tu na

Kuanzia Kushoto Katibu wa Bongo Movie Mkoa wa Mwanza Mr Kim , anefuata ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Dada Anitha toka Mwanza, Anaefuata ni William Malecela, Anaefuata ni Mwenyenyekiti kata ya Bwawani, Steve Nyerere, Paul Makonda na Mwenye Baragashia pale ni Mwenezi kata hii

Msanii mkaanga sumu akitumbuiza wananchi hawa

Furaha ikizidi mtu hushindwa kijizuia

mkaanga sumu akitema sumu

Furaha ilitawala eneo hili

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger