Home » , » Ridhiwani Kikwete ajibu Tuhumu zake Dhidi ya Vituo vyama Mafuta nk....!!

Ridhiwani Kikwete ajibu Tuhumu zake Dhidi ya Vituo vyama Mafuta nk....!!

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, June 18, 2014 | 2:14 AM

Inawezekana hili likawa moja kati ya maswali uliyonayo na hujawahi kupata nafasi ya kumuuliza muhusika au inawezekana ikawa ni ishu ambayo umewahi kuisikia au kuisoma kwenye chombo chochote cha habari.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview na millardayo.com anasema >>> ‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi’

‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger