Home » » Breaking News:- Ajali Mbaya ya Mabasi Yauwa Watu 16 Jioni hii

Breaking News:- Ajali Mbaya ya Mabasi Yauwa Watu 16 Jioni hii

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, August 19, 2014 | 9:59 AM


Ni Basi la SABENA na Basi la AM yamegongana

Basi la Sabena la Mbeya kwenda Mwanza na AM Dreamline ya Mwanza-Mpanda. Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 4 to wilaya ya Sikonge.
Mashuhuda wanadai takribani watu kumi au zaidi wamepoteza maisha wakiwemo madereva.
Maelezo baadhi ya mashuhuda wanadai dereva mmoja ameonekana kiwiliwili pekee na juhudi za kukisaka kichwa cha marehemu zinaendelea.
Wameongeza zaidi kuwa yawezekana hata madereva hao walikuwa ni Day-worker (Daiwaka) kama ilivyozoeleka.
Wakati mtandao huu ukipokea taarifa ni kuwa hali si nzuri eneo la tukio na uokoaji wa majeruhi zaidi ya 30 unaendelea na kuwapeleka katika hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.

Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.

Ajali Mbaya ya Basi yatokea Muda Si mrefu Wilayani Sikonge na Watu 16 wamefariki Papo hapo! Baada ya Basi la SABENA na AM kugongana uso kwa Uso!

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger