Home » , » Dk Hamisi Kigwangalla atangaza nia yakugombea Urais 2015

Dk Hamisi Kigwangalla atangaza nia yakugombea Urais 2015

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, September 7, 2014 | 10:40 PM

Picha zikionyesha matukio mbalimbali  kabla wakati na baada ya Mhe. Dr Hamis Kigwangalla mbunge wa jimbo la nzega kwa tiketi ya chama cha mapinduzi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa  mwakani kupitia chama cha mapinduzi ccm endapo kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya ccm kwenye kuwania urais ,akizungumza mbele ya waandishi wa habari asubuhi ya leo Dr kigwangalla alisema ameamua kutangaza nia ya kuwania urais  kwa maono yake mwenyewe kwa mapenzi mema kwa taifa la tanzania  na sio  kwa kushinikizwa na mtu yoyote nje au ndani ya chama chake,aidha alieleza kuwa nia yake ni kujenga Tanzania yenye uchumi uliotengamaa ukilinganisha  na kwa sasa  ambapo uchumi wa nchi haukuwi   kulinganisha na maliasili za nchi zilizopo   hazitumiki  kuimalisha uchumi wa nchi  na kujenga taifa lisilo na matumaini  huku wananchi wakikosa huduma  muhimu kama maji chakula huduma ya afya pamoja na miundombinu ya uhakika.alisema endapo atapewa nafasi  hiyo atajenga Tanzania yenye uchumi imara  yenye utawala bora pamoja na kuheshimu utu wa mtanzani ambao kwa sasa  umepoteza thamani yake .Dr kigwangwalla anakua kijana wa kwanza wa kitanzania ambaye alizaliwa tarehe saba mwezi wa nane  mwaka 1975 kutangaza nia ya kuwania urais hadharani bila woga, huku akijiamini kwa kiasi kikubwa akijibu moja ya maswali ya waandishi wa ha habari kuhusiana   kulitetea jimbo la nzega Dr kigwangwalla alisema nitaacha kutetea jimbo la nzega endapo chama kitanipa ridhaa ya kuwania urais  lakini kama chama hakitanipa ridhaa ya kuwania urais kupitia chama changu  nitagombea na kutetea jimbo la nzega kwa nguvu zangu zote.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger