Home » , » Jeshi la Polisi laonya wanaotumia vibaya mitandao yakijamii.

Jeshi la Polisi laonya wanaotumia vibaya mitandao yakijamii.

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, September 3, 2014 | 1:16 PM

Polisi waonya wanaotumia vibaya mitandao

JESHI la Polisi limewaonya watu wanaotumia mitando ya kijamii pamoja na simu za mikononi kusambaza taarifa za uchochezi,kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali, na watu mashuhuri kuacha tabia hiyo kwani ni kosa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alisema kuwa wananchi wanapaswa kutosambaza picha au ujumbe wowote wa uchochezi na ni vema wafute pindi wanapozitapata.

"Tumeshirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha wananchi wote wanazielewa sheria zote na elimu hii itakua endelevu ikiambatana na operesheni ya kuwabaini wote wanao fanya vitendo hivi"Alisema Bulimba

Aliongeza kuwa miongoni mwa makosa anayoweza kutenda mtu kwa ktuokujua au kujua ni pamoja na kutumia mtandao kwa ajili ya kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu,pamoja na kutuma na kupokea maneno ya vitisho na matusi kwa watu wengine

Alisema ni vema simu na mitandao ya kijamii ikatumika katika kuwasiliana na kupashana habari zenye mlengo wa kukuza maadili katika jamii.

"Serikali haikuleta Mkongo wa Taifa kwa lengo la kushusha maadili ya Taifa,lengo lilikuwa zuri la kufanya huduma ya mtandao kuwa nafuu na ya uhakika lakini cha ajabu ni kuona watu wengine wanatumia kwa manufaa ya kuzusha vitu ambavyo si vema jamii kuvijadili"alisema Bulimba.

Alisema tayari Jeshi la Polisi limesha washikilia baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo na takwimu sahihi za waliofikishwa mahakamani zitatolewa kwa vyombo vya habari pindi jambo hili litakapokamilika kisheria.
.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger