Home » » Katibu wa UVCCM Mkoa Morogoro Ndg Nicodemas Tambo Aendelea na Ziara Kata ya Gwata Wilaya ya Morogoro Vijijini

Katibu wa UVCCM Mkoa Morogoro Ndg Nicodemas Tambo Aendelea na Ziara Kata ya Gwata Wilaya ya Morogoro Vijijini

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, September 27, 2014 | 2:29 PM

Katibu wa uvccm mkoa wa mororogoro Ndugu Nicodemas M Tambo ameendelea na ziara yake katika mkoa wa morogoro kwa kutembelea wilaya ya Morogoro Vijijini Lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha kwa vijana wa Mkoa huo

Kukagua na kuimarisha uhai wa jumuiya , Kupanga mikakati ya ya kufanikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14/12/2014 , Kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kupiga kura, kuhamasisha vijana kugombea nafasi za uongozi, pamoja na kuhamasisha vijana kushiriki shughuri za maendeleo ili kujikomboa kiuchumi katibu wa vijana hakusita kusisitiza swala la maadili kwa vijana kwani ni moja kati ya malalamiko makubwa sasa Momonyoko wa maadili kwa kuwataka vijana kuzingatia maadili ya kitanzania na kutoshiriki katika vitendo visivyo vya kimaadili kwa watanzania ikiwa ni pamoja na uvutaji wa bange ulevi kupindukia na kushiriki katika ngono za umri mdogo

Ziara hiyo ililenga pia kufungua mashina ya wakereketwa pamoja na kupokea vijana walitoka vyama vya upinzani na kujiunga na chama cha mapindizi kugawa kadi kwa vijana wasio na kadi kukutana na vikundi vya michezo pamoja na kuchangia shughuri za maendeleo kwa vijana

Akiongea na mwandishi wa blog hii katibu wa vijana mkoa wa morogoro alifarijika kwa Mapokezi aliyoyapata mwitikio wa vijana walionao kwa viongozi wao "kitu nikichogundua wanachama wana kiu ya kukutana na viongozi wao hivyo naomba viongozi wa chama na jumuiya zote kushuka chini na kukutana na wanachama  hali hii huamsha ari kwa wanachama Lakini pia nawaomba viongozi wa chama na serikali kutoa ahadi ambazo wanaweza kuzitimiza maana kuna maeneo bado kuna kero za ahadi binafsi za viongozi nje na utekelezaji wa ilani" katibu wa vijana Mkoa wa morogoro alisema hakusita pia kusema anaamini vijana bado wana imani na chama cha mapinduzi na anaamini ushindi mkubwa katika chaguzi za serikali za mitaa na kuu..

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger