CHANZO NA CHOKOCHOKO ZA VURUGU TUNDUMA.
Mji mdogo wa Tunduma umegubikwa na ghasia toka siku ya j.3 - j.5.
Kisa ni eneo la plot lililoko mtaa wa makambini kata ya sogea
Toka mwaka 2009 alipochafuliwa m/kiti wa mtaa ndg Ally mwafongo (chadema) amekua akiuza maeneo mengi naya sababu ilyompa madaraka hayo nikwasababu kabla ya kuganyika na kuwa kata kilikua kitongoji hivyo kulindwa na sheria hiyo ya kitongoji na wanakitongoji kumiliki ardhi.
Baada yakuwa mtaa halmashauli ikaanza kupima maeneo ya wazi kwajili ya kupanga mji hivyo eneo la sogea lililowazi likapimwa na serikali na kugawa maeneo ya huduma za jamiii ikiwa soko eneo la ofisi za serikali ya mtaa n.k.
Eneojingine likakatwa ploti kwa matumizi ya binaadam na eneojigine bado liko wazi.
Mwiongoni mwa walioomba ploti ni ccm tawi la sogea nawatu wengine na ardhi wakakubali wakalipwa pesa na kutupatia ofer ya umiliki wa eneo.
Chadma wana ajenda ya siri wakaanza kuzusha kua eneo lile lote liko wazi hivyo ccm wamejilikisha kienyeji ndg. Ally akaipeka ccm balaza la kata kwakua ccm wanavielelezo vyote vya umiliki wa kiwanja Ally akashindwa kesi
Akakata rufaa ya mahakama ya ardhi ya wilaya pia kwakua hakua na vielelezo vyovyote pia kesi akashindwa na akatakiwa kulipa gharama za kesi ambazo mpakasasa hajalipa.
Hiyo juzi akaanzisha vurugu kwa kuwkusanya wafuasi wa chadema na kuwaambia tumeshinda kesi hivyo msingi uchimbwe tuanze ujenzi wa hospitali.
Baada ya tukio hilo wenye viwanja wakaenda kulipoti kituo cha polisi kua wamevamiwa maeneo yao nawatu wasiojulikana wakiongozwa na wenyeviti wa mtaa ya sogea.
Polisi watumia busara kubwa kwenda kuwaita viongozi wa chadema viongozi wa ccm na watu wengine wenye viwanja pamoja na watu wa ardhi.
Mimi nikiwa ni miongoni mwa viongozi wa ccm Tulipokaa polisi Ocd alitaka maelezo ya watu wa ardhi wamthibitishie nini tatizo?
Watu wa ardhi wakasema kama nilivyo eleza nawakatoa ufafanuzi zaidi kua eneo lile lilipimwa nandiomaana mkaruhusiwa kujenga soko na watu wakamilikishwa kisheria Afisa ardhi alienda mbali zaidi na kufafanua hilo wanalolitaka hao wanaoitwa wananchi kua wanataka hospitali akasema kama mnajenga hospitali ya serikari lazima mushirike serikli kwa hatua zote tangu kuomba eneo mkipewa lazima serikali iwape michoro ya majengo yake kwakua serikali ndio iatawaletea madawa,Daktari na manesi lakini jingine nchi nzima hospitali itajengwa kwenye kata nasii mtaa kama mnavyotaka ninyi tena mnadai lile ni eneo la serikali ya mtaa akasema kisheria mtaa haumiliki ardhi ila kitongoji na kijiji ndio wanamiliki ardhi kwasababu mtaa unakua mjini na mijini kunakua na kitengo cha mipango miji kilicho chini ya wizara ya ardhi.
Jingine akatueleza kua hospitali lazima itengewe eneo la zaidi ya heka moja na hili eneo mnalotaka kujenga halifiki hata heka moja hivyo mkitaka hospitali subirini ikiwakata ktk uchaguzi ujao. Au tumeni barua ya maombi tuwatafutie eneo.
Ocd akata kila mtu ajiridhishe kua ni eneolake halali ccm tukatoa vielelezo vyote vya umilikishwaji ardi barua ya maombi,kukubaliwa,malipo,na nyaraka za ofer,nawatu wengine pia wakaonesha.
Wanaosema wananchi wao hawana kielelezo chochote ocd akawataka japo waoneshe mukhtasari hata mmoja unaoonesha wanamtaa walikaa kujadili suala hilo pia hawana.
Japo walisema ukatafutwe hivyo tukakubaliana eneo lile liachwe kwanza ili na wenzetu wakalete vielelezo vyao nakila mtu akawaambie watuwake.
Siku inayofuatia wafuasi wa chadema sii wakaendelea na ujenzi tukatoa ripoti tena polisi bado Ocd akatumia busara akafika site na kuuliza kua jana tume.kubaliana vipi waliokuepo pale wakasema hawanataarifa hiyo ndipo ocd akamuita diwani Frank mwakajoka (chadema) kwamba awaambie watuwake yale tuliokubaliana jana maana wamesema hawana taarifa diwani akasema wananchi walikataa baada ya ocdbkuambiwa hivyo ndipo kikakunjuliwa kitambaa chekundu kuashiria amani imetoweka na polsi wakaanza kutangaza watuwote kuobdoka eneo lile baada ya nusu saa wengine walikaidi ndipo polisi walipotumia nguvu ya mabom ya machozi na virungu kuwatawanya diwani akaanza kuwatukana pilisi ndipo na yeye akaambulia kichapo na kuingizwa ndani ya gari la polisi nakupelekwa vwawa nawatu 25 waliokaidi amri halali ya polisi.
Baada ya wafuasi wa chadema kusikia diwani wao frank kawekwa ndani ndipo yakaanza maandamano nandipo polisi wakaongezwa ili kudhibiti vurugu zilizoanza kuzuka mji mzima
Mahakama inesema sheria haiogopi watu hivyo taratibu za mahakama zinaendelea tareh 30-3-2015 watatakiwa mahakamani.
HONGERENI JESHI LA POLISI KWAKUDHIBITI VEMA GHASIA ZILIZOZUKA NAWALIOKAMATWA SHERIA IFUATE MKONDOWAKE
MLIOFUATA MKUNBO LEO FAMILIA ZENU NDIO ZINAHANGAIKA KWA UPUMBAVU WA CHADEMA NA VIONGOZI WAO.
NA HATUTAKUBALI HAKI YA MTU KUPOTEA KWASABABU YA SIFA ZA KISIASA
HILI TUTALISIMAMIA MPAKA DAKIKA YA MWISHO.
NB:
WATANZANIA NADHANI MNAONA UONGOZI MBOVU WA HAWA WANAOJIITA CHADEMA
HAKIKISHA HAUWAPI NAFASI YOYOTE KWAKUWA HAWATAKI AMANI ILA VURUGU AMBAZO ZINAPELEKEA UVUNJIFU WA AMANI, UALIBIFU WA MALI NA KUPOTEZA UHAI AU KUJERUHI WATANZANIA.
SEMA NAIKATAA CHADEMA GENGE LA WAHUNI.
"BAKI NJIA KUU CCM, ACHANA NA MICHEPUKO YA UKAWA."
Post a Comment