Na. Magreth Kinabo
Jamii imetakiwa kudumisha utamaduni wa kuendelea kusaidiana kulea ndugu au watoto waliondokewa na wazazi wao ili kusaidia kupunguza idadi kubwa ya watoto wa mitaani na wale wanaotunzwa katika vituo mbalimbali nchini.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto DR KHAMISI KIGWANGALA wakati alipotembelea makao makuu ya Taifa ya kulea watoto Kurasini jijini Dar es Salaam kwa lengo kuangalia hali halisi ya matunzo ya watoto hao.
DK KIGWANGALA amesema pamoja na kwamba serikali imekuwa na jukumu la kuwalea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu lakini utamaduni uliopo kwa jamii wa kusaidiana kwenye majukumu mbalimbali ya kulea watoto usipouimarishwa kunaweza kusababisha wimbi kubwa la kulea watoto kwenye vituo mbalimbali.
Amebainisha kuwa pamoja na kwamba upo utamaduni huo lakini wazazi na walezi wanapaswa kuhakikisha kuwa wanadumisha familia zao na kuacha tabia ya kuwa na mifarakano ya mara kwa mara katika ndoa zao.
DK KIGWANGALA amesema wakati mwingine ukomvi au kutokuelewana kwa mara kwa mara husababisha kuwafukuza watoto katika familia hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha kuwa wanakuwa na maelewano mazuri ili kuweza kutoa malezi bora.
“ Nimeona hapa wapo baadhi ya watoto ambao wamekimbia majumbani kwao kutokana na kukosa malezi bora ambayo yangeweza kumvutia na kuendelea kuishi na wazazi wake lakini kutokana na malezi hafifu yamewafanya kutoroka makwao na kukimbilia mjini kutokuelewana kwa wazazi kunamfukuza mtoto,”alisema dk KIGWANGALA.
Aidha amesema jukumu la vituo hivyo ni kupokea watoto kwa muda kuwalea na kwa wale wenye wazazi serikali inaweka mpango wa kuwarudisha nyumbani kuwaunganisha na ndugu zao kwani mahali bora pa kukua mtoto ni kwenye familia.
Katika ziara yake hiyo naibu waziri huyo wa afya ameridhishwa na hali ya kituo hicho kwa madai kuwa amekiona kinaendelea vizuri na kina hatua zote muhimu wakiwemo wataalamu kubwa Zaidi ni kuhakikisha kuwa watendaji hao wanaboresha huduma Zaidi.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi wa makao hayo ya kulea watoto Kurasini ZAKA OLAIC amesema kituo hicho hivi sasa kituo hicho hakina dereva hata mmoja hali inayowawia vigumu kuwakuwapeleka na kuwarudisha watoto shuleni hasa wenye ulemavu na kumuomba Naibu Waziri kuwapatia madereva kwani magari yapo hayana madereva.
OLAIC amesema kinahudumia wato 72 wakike 36 na wakiume 36 kinalea kuanzia umri wa miaka miwili ambao baadhi yao wapo waliotoroka nyumbani na wengine kutelekezwa na wazazi ila wakifikaumri wa miaka 18 wanarudishwa katika familia zao.
MWISHO.
Post a Comment