👉🏿Karibu katika Dawati la Mwalimu Nyange la NAJUA WAJUA Leo 06/01/2016
👉🏿Habarini za Asubuh wapendwa woote
🙋🏾🙋🏾🙋🏾🙋🏾🙋🏾✋🏿✋🏿✋🏿
👉🏿Leo Dawati limejikita zaidi kwenye swali linaloendana na zama za sasa, zama za vijana,vijana wa kileo wa kidigitali, kizazi kipya cha sasa" JE TUNAOWA MWANAMKE KWAAJILI YA UJENZI WA FAMILIA BORA AU TUNAOWA MREMBO WA FAMILIA???? "
👉🏿Swali langu kuhusu kivutio chetu kwa mwanamke limejikita
Kwenye hoja ya kitu gani wanaadamu hutufanya tupende mambo Fulani na tuepuke mambo mengine???
👉🏿Socrates ,mwanafalsafa mashuhuri wa maadili anatuambia kuwa,"yeyote ambae hutenda,hutenda chini ya mtazamo wa kupata mazuri"
👉🏿Hivyo tendo lolote lile juu ya kitu Fulan hutendwa kwa sababu ya kupendwa kwa tendo hilo katika mazuri yake.
👉🏿Kwa mantiki hiyo, uono wa chema wa kitu ndio utoao tamaa juu ya kitu hicho.Kwa hiyo, utamanio( desire)unaweza kuelezwa kama ni tabia ya uelekeo kwa vitu vizuri vya kimwili au vya kihisia ambavyo, yule atamaniye hana("Desire could be described as a tendency towards a sensible good that is absent")
👉🏿Hivyo kwa mfano, mvulana au mwanaume anaweza tu kumtamani msichana au mwanamke pale tu ambapo anaona kitu fulani kizuri ndani ya huyo msichana au mwanamke.
👉🏿Ni hicho kizuri ndicho ambacho huvuta hisia zake kwake na hivyo hupelekea kutaka mapenzi.
👉🏿Mwanafalsafa Hobbes anasema , "binaadamu wanavutwa na kile ambacho wanachofikiri kuwa kitawasaidia kuishi na kuchukia kile ambacho wanakiona kinatishia usalama wa maisha yao"
👉🏿Dawati la Mwalimu Nyange limekuwa likijiuliza maswali mengi sana mfano HIVI WANAUME WANAOWA MWANAMKE KWAAJILI YA UJENZI WA FAMILIA BORA AU WANAOWA MREMBO WA FAMILIA???? pamoja na
✒Hivi Mwanamke tunamuoa kwa Mtazamo wa kupata mazuri au kwa Weupe wake????
✒Hivi kitu kizuri tunachokiona ndani ya mwanamke ni Sura nzuri alonayo ambayo sura hiyo itahakikisha watoto wanalelewa kwa kupenda kujisomea wenyewe nyumbani kuliko kupenda Tution inayoweza kuwaharibu watoto kulingana na mazingira wanakosomea na watu wanao kutananao huko.
👉🏿Hivi unajua Tathmini ya Hobbes inaonyesha kukamata hali halisi ya maisha yetu ya kila siku.
👉🏿Hivi wajua Mara kwa mara tunachagua Serikali ile ambayo tunaamini kuwa itatuletea kitu fulani kizuri. Ni serikali ya aina hii ndio tunayoipenda na tunayoifurahia.
👉🏿Hivi wajua Maneno ya Hobbes yananifanya nijiulize maswali haya
✒ ✒Mwanamke mwenye Makalio makubwa ambayo huonekana ni kivutio na kishawishi kikubwa kwa vijana kwa mapenzi na Ndoa ndio huleta kitu gani kizuri kwa familia.
✒Hivi unajua ukubwa wa makalio ya mwanamke hauwezi kuwalea watoto wakafahamu huyu ni mtu mzima anahitaji kusalimiwa, kupokewa mzigo inapobidi
✒Hivi unajua Ukubwa wa makalio hauwezi kuwalea watoto wakajua sasa tumeshakuwa majukumu yangu kama msichana ni haya na majukumu yangu kama mvulana ni haya.
✒Hivi unajua ukubwa wa makalio hauwezi kumlea mtoto akajua bangi,madawa ya kulevya, umalaya, ushoga nk ni kinyume na maadili
✒Hivi unajua uzuri wa sura ya mwanamke,u black beauty wa mwanamke,miguu minene ya mwanamke,u portable wa mwanamke,ukubwa wa makalio wa mwanamke na nk haviwezi kuilea familia yako katika misingi bora na imara ya kifamilia ispokuwa chagua mwanamke ambae atakuwa mganga,kiongozi, mlezi,mlinzi na mwokozi wa familia yako kwenye maandalizi ya kwenda kuishi vema na jamii yote na kuwa msaada kwa jamii na sio kero kwa jamii kwa lugha zao za matusi,mavazi yao yasiyo na stara,uhuni na tabia zote za ajabu kutokana na kukosa mlezi bora wa maisha yao ya familia sababu Baba hakuoa mama wa familia ambae ni mjenzi thabiti bali Baba aliowa MREMBO WA FAMILIA alieacha majukumu yake kwa wanawe akawa anakimbizana na anasa za Dunia.
👉🏿Hivi unajua kuna UJUHA mkubwa sana unaofanywa na vijana wa kileo kwenye mitandao ya kijamii, UJUHA huo ni
✒Kutoa picha na kusema anaetaka mapazia tuwasiliane alafu mbele ya mapazia kuna dada mwenye Makalio makubwa huo ni UJUHA
✒Kuuliza eti simu hiyo ni tekno au Smartphone pembeni ya bint aliekaa mwenye Makalio makubwa huo ni UJUHA
✒Kuuliza hivi hili gari ni aina gani halafu mbele ya gari amesimama au kukaa bint mrembo sana huo ni UJUHA.
✒Kuuliza hili jengo linajengwa na matofali mazuri hali ya kuwa kuna dada mrembo mwenye Makalio makubwa amesimama akiwa kajifunga khanga tu kama anatoka kuoga huo ni UJUHA.
✒Kuonyesha kontena lililopotea lileeeeee👉🏿Wakati lengo lako ni kutuonyesha bint alosimama pembeni mwenye Makalio makubwa huo ni UJUHA.
✒Kuuliza kumbe daraja la kigamboni ni la mbao?? Wakati kuna binti aliesimama kwenye Daraja hilo mwenye makalio makubwa huo ni UJUHA
👉🏿Hivi unajua mwanamke haolewi kwa hisia bali kwa malengo na usimamizi bora
👉🏿Hivi unajua kuwa mwanamke unaemuoa leo kwa ashki ya hisia anaweza kubadilisha ndoto zako zikapotea na kutoa furaha yako ya maisha na kuingia kwenye maumivu ya moyo na akili ukaiona Dunia mbaya???? Kuwa mwangalifu, OWA MAMA MJENZI WA FAMILIA NA SIO MAMA MREMBO WA FAMILIA.
👉🏿Owa mke mzuri wa moyo,akili,maadili familia yako inufaike na uzuri wa sura,rangi,umbile na ukubwa wa makalio iwe sababu ya nyongeza na isiwe ndio sababu ya msingi ya kuowa.
👉🏿Hivi unajua kuwa ni muhimu sana tena sanaaaaaa kufuatilia historia ya mtu unaetaka kumuoa,malezi na makuzi yake alokulia,familia yake ilivyo kama niyawema au shari, kazi anayofanya,maumbile yake kama anaakili vizuri, busara,uoni wa mbele wa maisha kuliko kuzingatia na kuvutika kwa Makalio makubwa, uzuri wa sura, umbile,sauti,mwendo au utajiri wake au ufahari wa familia yake.UTAKUJA KUJUTA
👉🏿Hivi unajua msomi na mwanafalsafa mmoja mkubwa Duniani akiitwa Muhammad ibin Abdullah bin Abdulmutwalib aliwahi kusema kwenye miaka ya 623AD kuwa "wanaume hupenda kuoa mwanamke kwa mambo manne ambayo ni mali yake,nasaba yake,uzuri wake na Dini yake" lakini alisisitiza sana,sana sana kuwa mwanamke mzuri kumuoa ni yule atakaeolewa kwa Dini yake,na wala sio ukubwa wa makalio wala u black beauty wala u portable wake wala uzuri wa sura na umbo.
akiamini kuwa mwanamke mwenye Dini atakuwa ni mama Mjenzi bora wa familia na sio mama mrembo wa familia.
👉🏿Hivi wajua ukitaka kumjua msomi huyu MKUBWA wa mwaka 623AD ingia kwenye Google andika "THE 100 :RANKING OF THE MOST INFLUENTIAL PERSONS IN HISTORY by MICHAEL H.HART"
👉🏿Jumaa tano njemaaa
👉🏿Toa mchango wako kwa Taifa lako
👉🏿Weka kumbukumbu muhimu kwa jamii yako ya leo na kesho ikukumbuke na usiwepo Duniani kwa kuwa ulizaliwa tu.
👉🏿Tumia akili siku moja historia iseme nawe ulikuwepo.
👉🏿Endelea kufuatilia dawati la Mwalimu Nyange la NAJUA WAJUA hapo kesho tar 07/01/2016
👉🏿Nawatakia Asubuh njema wadau nawapenda sana sana aaaaaaaaaa wadau nawapenda
✋🏿✋🏿✋🏿🙏🙏🙏🙋🏾🙋🏾🙋🏾👍🏿👍🏿👍🏿
Home »
kitaifa
» Je! Tunaowa mwanamke kwa ajili ya ujenzi wa Familia bora au tunaowa Mrembo wa Familia!
Je! Tunaowa mwanamke kwa ajili ya ujenzi wa Familia bora au tunaowa Mrembo wa Familia!
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, January 5, 2016 | 9:57 PM
Labels:
kitaifa
Post a Comment