👉🏿Karibu katika Dawati la Mwalimu Nyange la NAJUA WAJUALeo 05/01/2016.
👉🏿Habarini za Asubuh wapendwa woote
👉🏿🙋🏾🙋🏾🙋🏾✋🏿✋🏿✋🏿
👉🏿Leo Dawati limejikita kutukumbusha juu ya swali, JE "UPUMBAVU NI KIPAJI KAMA ILIVYO UFUPI NA UREFU???"
👉🏿Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere aliwahi kusema "Upumbavu ni kipaji "
👉🏿Hivi unajua mtu anaweza kuzaliwa nacho(kipaji cha Upumbavu)na anaweza kufa nacho.
👉🏿Hivi wajua Mpumbavu ni tofauti na mtu mjinga???
👉🏿Hivi unajua mtu mjinga anaweza kueleweshwa,kuelimishwa akaelewa na ujinga wake ukafutika.!!!
👉🏿Hivi unajua bado najiuliza ni kwa nini baba wa Taifa katika mazungumzo yake sikumoja alisema,....... Upumbavu ni kipaji kama ilivyo urefu na ufupi"
👉🏿Hivi wajua Nnachotaka kusema, kwa miaka yote tangu uhuru tumetumia nguvu nyingi sana kupambana na vita dhidi ya ujinga na kusahau vita ya Upumbavu.
👉🏿Hivi unajua ndio maana pamoja na kuwa na wasomi wengi kwenye Taifa letu bado Upumbavu unaligharimu Taifa letu.
👉🏿Hivi wajua Ujinga ni Ugonjwa na wakati Upumbavu ni Utashi wa Mtu mwenyewe.
👉🏿Hivi wajua ni vigumu kumwelewa Mwalimu Julias Nyerere pale aliposema Upumbavu ni kipaji kama ilivyo urefu na ufupi.
👉🏿Hivi unajua Upumbavu wa watu wasiojali, wasio na dira, wasio na huruma,wasioona mbele,wasio na uono wa Tanzania ijayo ndio umepelekea baadhi ya madaktari kuhatarisha afya zetu,baadhi ya wanasheria kuchezea haki zetu,baadhi ya wanahabari kupindisha ukweli, baadhi ya wana Dini kuharibu maadili,baadhi ya wasimamizi wa elimu, na waalimu,waalimu,waalimu,waalimu kuvuruga elimu yetu na nk,ndio maana wajua nimefikiri baada ya kupambana na ujinga,maradhi na umaskini kwa muda mrefu sasa pia tuongeze kupambana na UPUMBAVU.
👉🏿Hivi wajua kumbe Upumbavu ni hali ya kufanya kosa huku ukijua kabisa ni kosa na unafanya kwa makusudi.
👉🏿Hivi unajua makusudi haya maranyingi husukumwa na ile dhana ya Niccolo Machiaveli ya "The End Justifies the Means"na hali hii haiwezi kuondolewa hata kama unaelimu kubwa kiasi gani,maana nikipaji.
👉🏿Hivi unajua Socrates aliwahi kusema "to know is not to act"akiwa na maana kujua siyo kutenda, ndio maana nchi yetu inawasomi wengi wanaojua mengi lakini hawatendi kulingana na Ueledi wao.
👉🏿Hivi wajua wasomi wanaongezeka, wizi unaongezeka kwa tamaa ya kumiliki maisha ya ufahari kwa jasho lisilostahiki,uzalendo unatoweka, huruma inayeyuka,wadau tusipobadilika Nchi itaangamia kwa miaka 50 ijayo.
👉🏿Hivi wajua Dawati la Mwalimu Nyange linashauri
✒ tusipende kupata mafanikio pasipo kufanya kazi halali kwa bidii.
✒Tusiwe mashabiki kwa mambo tusoyajua au kuwa na hakika nayo badala ya kuwa watendaji na washauri wa dhati kwa maendeleo ya Taifa .
✒Tusipende mabadiliko ambayo nafsi yako kwa matendo yako bado haijabadilika.
✒Tusihukumu bila kuwa na hakika ya dhati kwa uambiwalo.
✒Fanya unalodhani ni jema na litaacha athari chanya kwa jamii ya sasa na baadae .
👉🏿Toa mchango wako kwa taifa lako.
👉🏿Weka kumbukumbu muhimu kwa jamii yako ya leo na kesho ikukumbuke na usiwepo Duniani kwa kuwa ulizaliwa tu.
👉🏿Tumia akili siku moja historia iseme nawe ulikuwepo.
👉🏿Endelea kufuatilia dawati la Mwalimu Nyange la NAJUA WAJUA hapo kesho tar 06/01/2016 Nawatakia Asubuh njema wooooooote. ✋🏿✋🏿✋🏿🙏🙏🙏🙋🏾🙋🏾🙋🏾Nawapenda sana sana aaaaaaaaaa wadau nawapenda.
Post a Comment