Home » , » Mansour Yussuf Himidi apewa Pasipoti visivyo Halali kuihujumu Zanzibar

Mansour Yussuf Himidi apewa Pasipoti visivyo Halali kuihujumu Zanzibar

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, January 5, 2016 | 6:03 AM

Na;-
Hajji Nyanya.

"HUENDA MANSOUR YUSSUF HIMIDI APEWA PASIPOTI VISIVYO HALALI KUIHUJUMU ZANZIBAR '' 

                AFISA wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, Subira Maulid amehusika na njama za kumpatia hati ya kusafiria watu mashuhuri (Diplomatic Passport), kinyume na taratibu za kisheria aliyewahi kushikilia nyadhifa mbali mbali za SMZ ikiwemo  Waziri wa Kilimo  Mansour Yussuf Himid.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuamini vya habari hizi kutoka ndani ya ofisi za Idara hiyo Z’bar, zinaeleza kwamba Mansour alikuwa akimiliki Hati hiyo ya kusafiria( Diplomatic Passport) yenye no. AB708047 iliyokuwa ikimpatia uwezo wa kusafiri nje ya nchi kwa nafasi yake ya uwaziri.

Chanzo kimesema baada ya Mansour kufukuzwa ndani ya chama chake cha CCM na baadae kuvuliwa nafasi ya uwaziri aliirejesha Diplomatic Passport  katika idara ya uhamiaji Zanzibar kama sheria inavyoelekeza.

Katika hali isiyotarajiwa chanzo hicho kimethibitisha kuwa  Mansoor alichukua tena Passport hiyo kinyume cha sheria na alifanyiwa Mipango na kupewa na Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar anaejulikana kwa jina la Subira Maulid  ambae ni Mke wa Mohamed Mughiery (Eddy Riyami)  na kuitumia kwenda Africa kusini kutengeneza mipango ya kupata karatasi za kura zilizotumika huko kisiwani pemba na ambazo pia zilizosababisha uchaguzi wa octobar 25 kufutwa.

Baada ya kurudi Africa kusini na kumaliza jukumu alilopewa na chama chake  cha CUF na kulifanya kwa ufanisi mkubwa, Mansoor aliirejesha Passport hiyo kwa Bi. Subira  Maulid ambaye ni Afisa Uhamiaji Zanzibar,  aliyempatia Passport hiyo kinyume cha sheria.

Aidha hali hiyo imeendelea ambapo Mansour amepewa tena passport ya kawaida (Ordinary Passport) na Bi. Subira ambae pia ni mke wa rafiki yake Mansoor na inaaminika baada ya wiki mbili kuanzia sasa atasafiri kuelekea nchi mbalimbali za nje zikiwemo za kimagharib kwa lengo la kuzishawishi ili kuwasaidia katika mipango yao ya kuanzisha vurugu Zanzibar.

Afisa huyo wa idara ya uamiaji Z’bar Subira Maulid amekuwa akivunja sheria za nchi na maadili ya kazi yake kwa makusudi kwa lengo la kuwasaidia viongozi wa ngazi za juu wa CUF kusafiri kinyume na sheria kwenda nje ya nchi kutengeneza mitandao haramu ya kuharibu na kuhujumu Amani na utulivu wa Z’bar.

Je tujiulize Mansoor, Ismail Jussa, Eddy Riyami, Subira ambae ni afisa wa Uhamiaji na Maalim Seif wanania njema na Zanzibar? Je vurugu zitakapoanza Zanzibar wananchi wa cuf watakuwa salama hawatauwawa? Je nchi ikiwa kama Sudan, Somalia na Libya Maalim Seif na timu yake watafaidi kitu gani? je hiyo ndio Singapore  ijayo?.

Nitaendelea kusema,huu ni uhuru wangu wa kikatiba!..







Wako,
Hajji Nyanya .

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger