UVCCM washupalia mali zao zisiguswe.
Na mwandishi Wetu.Kibaha
Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani imesema itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayevamia shamba la umoja huo lililopo kijiji cha Nyanzula Kata ya Kibaha mkoani humo.
Umoja huo umesema shamba hilo linamilikiwa kisheria na jumuiya hiyo baada ya kupimwa na kupatiwa hati ya umiliki kwa mujibu wa sheria za nchi.
Katibu wa Uvccm Mkoa Pwani Pili Augostino amesema hayo jana wakati wa ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka kulitembelea shamba hilo lenye ekeri 56 wilayani Kibaha
Pili alisema uvccm haitamvumilia mtu au kuionea aibu taasisi yeyeto itakayovamia shamba hilo aidha kwa ajili kilimo au kujenga majengo na makaazii ya kudumu
"Niinakuhakikishia Katibu Mkuu shamba hili na mali au rasilimali zote za uvccm hazitatumiwa kwa maslahi binafsi au kupotea kiholela, tuko makini na hatulala wakati wote "alisema katibu huyo.
Aidha alisema ofisi yake imehakiki mali zote za uvccm na sasa ziko katika orodha maalum katika mikono salama na hatatokea mtu yeyote kuiba au kudhulumu.
Kwa upande wake Mkuu wa Utawala wa Umoja wa Vijana wa CCM toka Makao Makuu Omar Mwanang"walu amewataka makatibu wote wa uvccm mikoa, wilaya na kata kuhakikisha mali za jumuiya hiyo hazitumiwi kwa maslahi binafsi.
Mwanang"walu alisema rasilimali na mali za chama na jumuiya zake ndiyo uhai na utii wa mgongo kwa maendeleo yake katika maisha ya siasa na ustawi wake.
"Wanaofiiri mali za chama shamba la bibi au zizi la mifugo lisilo na muangalizi au mnyapara , anajidanganya kwasababu kila aliyetenda na atakayetenda atakumbana na mkono wa kanuni za jumuiya na sheria za nchi " alisema.
Alisema kila mtendaji katika ngazi yake kwa kushirikiana na vyombo vyenye dhamana ya kikatiba katika uvccm ni wajibu wao kulinda, kuhifidhi na kutunza mali za jumuiya hiyo.
Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka yuko katika ziara ya kiutendaji akikutana na makatibu wa mikoa na wilaya katika jumuiya hiyo ambapo hadi sasa amepita katika kanda ya mashariki, kati na nyanda za juu .
End
Post a Comment