Watumishi wa sekta ya afya watakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu
Hayo yamesemwa leo na Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,dkt. Hamisi Kigwangwala wakati akitembelea hospitali ya mount meru mkoani arusha
Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe Kwa ukusanyaji was mapato,hivyo ipo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao utawafanya watu Wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi
"Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapo
Aidha,dkt.kigwangwala alisema licha ya serikali kupata pesa,watoa huduma pia wakiwemo madaktari,wauguzi pamoja na kada zingine kupata motisha ambazo zitawafanya kuwapa moyo wa kuwahudumia wagonjwa law hali na Mali.
"Kama matajiri hawaji kwenye hospitali Za umma,mnategemea hawa maskini watapata pesa wapi za kulipia huduma?aliuliza.
Hatahivyo naibu waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma Kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma,dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko pa kulipia
"Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma Za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma was serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi
Watumishi wa sekta ya Afya watakiwa kuwa wabunifu ili kitoa huduma kwa watu wote.
Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, January 30, 2016 | 5:19 AM
Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,dkt.hamisi kigwangwala(katikati) akizungumza na viongozi wa hospitali ya mount meru mara Banda ya kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali hilo,kulia ni mganga mkuu was mkoa dkt.Frida Mokiti na kushoto Nina mganga mfawidhi wa hospitali hiyo dkt.Jackline Urio
Dkt.kigwangwala amembeba mtoto mchanga(hajapewa Nina bado) wa bi.jamila petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
Naibu waziri huyo akimuangalia mtoto huyo
Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa,dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali,kushoto ni mtaalamu wa viwango cya maabara,Felix zelote,akimpatia maelezo waziri huyo
Labels:
kitaifa
Post a Comment