Home » » Habari ya Meya wa Kinondoni na aliekuwa Mgombea Urais UKAWA Ndg Lowassa Wameshindwa kudhibiti Speed ya DC Paul Makonda Kinondoni.

Habari ya Meya wa Kinondoni na aliekuwa Mgombea Urais UKAWA Ndg Lowassa Wameshindwa kudhibiti Speed ya DC Paul Makonda Kinondoni.

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, February 22, 2016 | 9:09 AM

Kutokana na kile kinachosemekana kuwa Meya wa Kinondoni na aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Ukawa,Kushindwa  kudhibiti Speed ya Makonda sasa wameanza mashambulizi binafsi tena yasiyokuwa na faida kwa wanakinondoni.

Hofu yao kubwa ni uwezo wa Makonda kukaba kila kona kwa kuwatafutia maendeleo wananchi huku wao wakijipanga kuwapa tenda wafanyabiashara waliowachangia kipindi cha uchaguzi na ndyo maana Meya anamwogopa Makonda kiasi kwamba anahisi mikataba kama ile ya Richmond haitapenya kinondoni. Ona ulishawahi ona wapi Meya anakataza watumishi wa Manispaa hata wasisalimiane na mkuu wao wa Wilaya mbaya zaidi hata Madiwani wa ukawa wameambiwa wakiwa na shida wasiende kwa Makonda. Ikumbukwe Ukawa walisema hawataki mikataba ya siri Leo Makonda kuwajuza wananchi  mambo ya maendeleo ametowa Siri.  

Wataalamu wa mambo wanasema Meya huyo anaendeshwa na mgombea wa urais kiasi kwamba hakuna hata Diwani mwenye kusema jambo likakubalika kama Nywele nyeupe hajaagiza . Sasa kwa mtindo huu tunaweza  kurudi kwenye Enzi za kina Mgeja na Msindai walipokuwa wenyeviti wa ccm na Kushindwa kufanya kazi zao kama viongozi bali ni watu wa kupokea maelekezo kwa nywele nyeupe.  Maswali yangu kwa Meya.

1) Kunaubaya gani Makonda kuomba support ya wadau ili ajenge secondary kwa ajiri ya Vijana tena zaidi 3183 wakiwemo na wakata ya Ubungo. Ambapo wewe umekuwa Diwani kwa miaka mitano na haujawajengea,matokeo yake watoto wanaenda kusoma kata za wenzako?

2)kosa lipi kwa Makonda kukutana na Wenyeviti wa mitaa wakati wenyeviti wa mitaa ni wenyeviti wa kamati za ulinzi kwenye mitaa yao.

3) tumeona Mabalozi mbalimbali wakienda kutembelea Makonda je ulitaka awaeleze Mabalozi hao mambo gani kama siyo changamoto za wanakinondoni

4 ) Ulikuwa Diwani mlichukuwa hatua gani za kutatua changamoto za ardhi mpaka ujisikie vibaya Makonda kutumia vipaji vyake kuwasaidia wananchi.

5) unaponda kazi ya vipaji mbona tumemwona mzee wako akiwa na wasanii kwenye campaign zake ila Makonda kuanzisha mashindano ni kosa.

6) unawasifia wahandisi waliofanya ufisadi na kutujengea barabara mbovu tena kila mwaka na kumponda Makonda kwa kazi ya uchunguzi tena iliyoleta majibu ya kitaalam kuwa tunaibiwa wewe kwako huoni mateso  wanayoyapata wananchi kwenye hizo barabara?

Yako Mengi ila ushauri wangu kwako Meya wa kinondoni ebu tumikia wananchi usiendeshwe na huyo aliekataliwa na wananchi.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger