Home » » DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.

DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, April 25, 2016 | 7:11 AM

DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo ametembelea ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco kuona maendeleo yake. Barabara hiyo ambayo ilikua na kero kubwa ya foleni iliamriwa kupanuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika hatua yake ya kubana matumizi na kupeleka fedha katika shughuli za maendeleo.
Katika ziara yake hiyo Mh. Hapi alitembea umbali wa mita 500 kwa miguu kukagua pia usafi wa mazingira ya kando ya barabara ambapo alipofika katila kituo cha mafuta cha Total, aliagiza uongozi wa kituo kufanya usafi wa mazingira yaliyo mbele ya kituo chao.
Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya pia alizungumza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Mkandarasi na wataalam wengine wa ujenzi na kujua maendeleo yao.
Meneja wa TANROADS na Mkandarasi walimueleza Mkuu wa wilaya kuwa tayari kazi imekamilika kwa asilimia 90 na kwa mbali wanatarajia kukabidhi mwezi June mwaka huu.

DC akihoji Jambo
DC akizungumza na Wataalamu wa Barababara
Mh DC Akipewa maelekezo nakutizama wafanyakazi wavyonyomya Maji yaliyojaa ktk Sehemu ya Barabara hiyo inayotakiwa kutengenezwa.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger