Wilaya ya Monduli yazindua umezaji kingatiba ya ugonjwa wa vikope(Trakoma)
Wananchi wa kijiji cha Meserani wakisikiliza hotuba toka mkuu wa wilaya (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa umezaji wa kingatiba za ugonjwa wa trakoma uliofanyika kwenye kitongoji cha Losingirani
Dkt.Upendo Mwingira(mwenye nguo burgundy) akimpatia kingatiba Mkuu wa Wilaya ya Monduli Francis Miti
Mama wa boma bi.Himayo Merio (aliyeshika kikombe)akipokea kingatiba toka Kwa mhudumu wa afya ngazi ya jamii bi.Jamila Karanga.zoezi hili linafanyika katika jamii hiyo kwa kuwatembelea kaya kwa kaya
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Francis Miti akihutubia wanakijiji wa kijiji cha Meserani juu(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa umezaji kingatiba ya ugonjwa wa vikope(trakoma),kulia ni Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamio,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Upendo Mwingira
Mwenyekiti wa kijiji cha Meserani juu,Ngimasirwa Silalee akimeza dawa kwenye uzinduzi huo,kulia ni mkuu wa wilaya ya monduli
Kikundi cha ngoma cha akina mama wajasiriamali cha kimasai wa kijiji hicho wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa umezaji wa kingatiba ya Trakoma
Diwani wa kata ya Meserani Mhe.Loti Naparana akimeza kingatiba ya Trakoma(Zithromax)wakati wa uzinduzi huo
Mmoja wa mtoto katika boma la mzee Sanare Midimi wa kitongoji cha Losingirani akinyweshwa dawa iliyopo kwenye mfumo wa maji maalum kwa watoto wadogo
(Picha zote na Catherine Sungura-Wizara ya Afya)
Post a Comment