Home » » DC WA KONGWA APIGA MARUFUKU WAFANYABIASHARA KUINGIA VIJIJINI KUNUNUA MAZAO PIA AMETOA SIKU SABA KWA WATENDAJI KUHAKIKISHA JENGO LA SOKO NA GHALA LA MAZAO KUANZA KUTUMIKA.

DC WA KONGWA APIGA MARUFUKU WAFANYABIASHARA KUINGIA VIJIJINI KUNUNUA MAZAO PIA AMETOA SIKU SABA KWA WATENDAJI KUHAKIKISHA JENGO LA SOKO NA GHALA LA MAZAO KUANZA KUTUMIKA.

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, August 3, 2016 | 1:23 PM

DC WA KONGWA APIGA MARUFUKU WAFANYABIASHARA KUINGIA VIJIJINI KUNUNUA MAZAO PIA AMETOA SIKU SABA KWA WATENDAJI KUHAKIKISHA JENGO LA SOKO NA GHALA LA MAZAO KUANZA KUTUMIKA.
 
Katika hali ambayo inaonekana kurudisha matumaini mapya kwa wananchi na hasa wajasiriamali Wa wilaya ya kongwa ni pale Mhe.Mkuu Wa wilaya hiyo DEOGTRATIUS NDEJEMBI alipotembelea eneo hilo La soko lililopo wilayani humo Kata ya Mkoka Tarafa ya Zoisa ili kujionea namna gani shuguli za maendeleo na ujasiliamali zinavyokwenda, Lakini tofauti na mategemeo yake mkuu wa wilaya hiyo alikutana na jengo tupu lililozungukwa na nyasi ndefu ikiashiria hakuna shuguli yoyote ya kibiashara iliyowahi kufanyika kwenye jengo hilo Tangu ujenzi wake ulipokamilika, Ndipo mkuu Wa wilaya akang'aka mbele ya watendaji Wa wilaya hiyo na kata ya mkoka kutaka kujua kwa nini Jengo hilo halitumiki licha ya kugharimu pesa nyingi katika ujenzi wake ambapo kiasi cha Tsh 56,000000 Million zilitumika kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo ambalo Tangu ujenzi ulipokamilika hadi Leo ni Takribani miaka 3 sasa ambapo soko hilo lilijengwa kwa nguvu ya wananchi na mapato ya halmashauri.
Kwa muda mrefu sasa wananchi wa kongwa kata ya mkoka imekuwa ni kilio chao soko hilo kutumika lakini halmashauri imekuwa haichukui hatua zozote zile na kuacha jengo likichakaa bila kutumika na wananchi wakiteseka Kwa kukosa maeneo ya kuuzia na kununua mazao yao licha ya kwamba Eneo hilo ndo linalozalisha mahindi kwa wingi sana katika wilaya ya kongwa, Mbali na jengo hilo na ghala kutokutumika Mkuu wa wilaya hiyo amegundua kuna wizi mkubwa umefanyika kwenye hatua za ujenzi wa  jengo hilo kwa ujenzi kufanyika Chini ya kiwango tofauti na fedha zinazodaiwa kutumika,
MKUU HUYO WA WILAYA AMETOA MAAGIZO KWA WATENDAJI WOTE WA HALMASHAURI KUHAKIKISHA HAKUNA MFANYABIASHARA YEYOTE ANAYEINGIA VIJIJINI KUNUNUA MAZAO NA ATAKAYEBAINIKA AKAMATWE NA KUPELEKWA POLISI
LAKINI PIA NDANI YA SIKU SABA SOKO HILO LIANZE KUTUMIKA ILI WANANCHI WAPATE FURSA YA KUUZA NA KUNUNUA MAZAO YAO KWA UHAKIKA LAKINI PIA KWA WAJASIRIAMALI WENGINE WADOGO KUPATA FURSA YA KUENDESHA BIASHARA MBALIMBALI NA HATIMAYE KUONGEZA KIPATO KWA WANANCHI KWA UJUMLA

NA MWANDISHI WETU
FIRES MEDIA🔥🔥🔥

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger