KONGWA, MH NDEJEMBI AVAMIA KITUO CHA AFYA MLALI WILAYANI KONGWA NAKUGUNDUA UJENZI CHINI YA KIWANGO WA JENGO LA UPASUAJI.
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deogratius Ndejembi, Mapema leo alikuwa na Safari ya kwenda Mlali kwa majukumu yakila siku, lakini alipofika mlali akaamua kukatisha nakuvamia Kituo cha Afya Mlali ambacho ni Kituo kikubwa chakutegemewa kwa Kata Nzima ya Mlali na Vijiji vya jirani.
Mkuu wa Wilaya alipofika kituoni apo alisaini kitabu kisha aliambatana na Mganga Mkuu wa Kituo hicho nakutembelea maeneo mbali mbali kituoni hapo ikiwemo Majengo, Wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa Kujengwa Chini ya Kiwango, Likiwa Dogo kiasi chakupelekea kushindwa kuweka Vitanda Humo Ndani.
Licha ya Hivo limejengwa Chini ya Kiwango na Jengo hili Lilijengwa Chini ya Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Kabla Mkuu huyo wa Wilaya hajateuliwa kutumikia wilaya hiyo.
DC kaagiza kuhakikisha Mkandalasi Atafutwe Mara Moja ili Kuhakikisha Jengo hilo Linalekebishwa na alirekebishe kwa kulijenga kwa Garama Zake Mwenyewe.
Mkuu huyo wa Wilaya Alimwambia Mganga Mkuu kuwa Nivema akawa Makini kuhakikisha Hospitali yake inakuwa na Huduma bora kwa ajili Kuhudumia Watanzania wa Mlale na maeneo ya Jirani Eneo hilo.
DC alizungumza na Wagonjwa waliokuwa Hapo nakutaka kujua Huduma kama wanazipata kwa wakati na Bora.
Majibu ya Wagonjwa ni kuwa Huduma ni Nzuri lakini Chanjo kwa Watoto wamekuwa hawazipati kwa wakati, haya yalisemwa na Wamama waliokuwa Kliniki hapo.
Na Ndipo Mkuu wa Wilaya alipoagiza kuhakikisha Chanjo hizo zinapatikana kwa Wakati na kama MSD wanawachelewesha kwa kuwaletea Dawa basi waseme! Majibu ya Mganga Mkuu ilikuwa MSD wanaleta kwa Wakati lakini changamoto ni watendaji tu!
Mkuu wa Wilaya kaagiza kuhakikisha Mapungufu hayo yanarekebishwa haraka iwezekanavyo.
Post a Comment