Home » » MKUU WA WILAYA YA KONGWA AMSIMAMISHA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI KONGWA.

MKUU WA WILAYA YA KONGWA AMSIMAMISHA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI KONGWA.

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, September 27, 2016 | 7:10 AM

MKUU WA WILAYA YA KONGWA AMSIMAMISHA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI KONGWA.

Mkuu wa Wilaya MH Deogratius Ndejembi Amefikia uamuzi huo Baada yakulalamikiwa na Wafanyakazi kwa Zaidi ya Mara Tatu.
Lakini pia Kikubwa Zaidi ni Swala la Meneja huyo kushindwa kusimamia Miundombinu ya Maji Wilayani Kongwa, Kumekuwa na Ugumu wa upatikanaji wa Maji kwa kiwango kikubwa sana, ivo kufanya swala la ukosekanaji wa Maji Kongwa kuwa Tatizo Sugu.

Lakini ni Kama Mwezi umepita DC alikwenda kwa ajili ya Kutatua Migogoro na alizungumza na Meneja huyo ili kuboresha nakumaliza kero Zao lakini wapi!

Ijumaa ya wiki iliyopita Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Kongwa waliandamana mpaka ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakiwa wamegoma kufanya kazi mpaka watakapolipwa Mshahara wao, Wafanyakazi hao wanadai Mishahara ya zaidi ya Miezi tisa (9) hawajawai lipwa tangu mwaka uanze.

Wakizungumza MH DC wafanyakazi hao wamemlalamikia kuwa, Mkurugenzi wao amekuwa akiwatukana kila wanapodai Haki yao. Mbali na hilo wamesema Mkurugenzi amewaambia Kama hawataki waache kazi kwani wapo watu wenye shida na kazi hiyo.

DC aliwaomba wurudi kazini na wamwambie  mkurugenzi wao kuwa anakuja kusikiliza kero zao huko nakutatua. DC alikwenda na Ajabu Mkurugenzi aliondoka mbali nakuwa alipewa taarifa za kuwa Mkuu wa Wilaya anamuhitaji kwa Kikao nae.
DC alifanya Kikao nakuomba kujua Mapato na matumizi na kugundua kuwa kila Mwezi wanakusanya zaidi ya Millioni kumi na Moja (11M) na kwamwezi wafanyakazi wao wanahitaji Kama millioni tano (5M) kwa malipo ya mishahara, lakini mkurugenzi kashindwa kuwalipa wafanyakazi wake.

Mbali na Hilo hesabu zinaonyesha kuwa yeye hajawai acha kulipwa mshahara na posho zote anajilipa yeye na fundi Mkuu wake wa Bomba Ambae alimuajili mwenyewe. Na wafanyakazi wamemlalamikia kwakuwa pia fundi mkuu huyo wa Bomba nae Hana adabu kwa wafanyakazi wengine.

Jana jumatatu Mkuu wa Wilaya kafikia uamuzi wakumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Maji Ndg, Kisha Bonga Leo kwa kuona hawezi tena kuitumikia mamlaka hiyo.
Kutokana na maamuzi hayo Mkuu wa Wilaya akishirikiana na Mkurugenzi Wamemteuwa Eng. Hamisi Ally kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Maji, na Mara tu Baada ya kukaimishwa jana Kaimu mkurugenzi huyo alianza kazi kwakuongozana na DC kwenda kata ya Chamkoroma kutatua kero ambayo imekuwa yakudumu huko kwa hujuma za wafanyabiasha ya Maji kukata Bomba nakujiungia wao ili wajaze madumu Yao na kuuzia wananchi kwa Shilingi Mia Nne kwa Dumu la lita ishirini.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger