MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC)- CHISALU
Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Mh Jabir Shekimweri, alipata Malalaniko toka kwa wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi - Chisalu wakihoji na kulalamika juu ya Mambo ambayo yana sintofahamu juu ya Hatma ya Masomo yao chuoni hapo.
Wanafunzi hao walikuwa na Maswali ya Msingi kwa Serikali ambapo,
Pamoja na Malalamiko Yao mengine, walihoji nakuomba wawasaidiwe juu ya Mambo haya:
1) Mbali na ukweli kua chuo chao ni chuo cha maendeleo ya Wananchi, Vipi Chuo chao hicho kudahili Fani ya Kilimo na Mifugo ni sahihi?
2) Wanapofanya Mitihani Mitihani yao hua nikutoka VETA sasa Kwa nini Wafanye Mtihani ulioandaliwa na VETA wakati mtaala wao sio wa VETA?
Mbali na hilo fani ya Kilimo na Mifugo haina nambari ya mitihani (exam code).
3) Je, wanaweza kuhakikishiwa ajira kama Maafisa Kilimo na Mifugo?
Akiwa anafuatilia na kutaka kujua nini hatma ya wanafunzi hao akasikia Chuo kimefungwa, Ndipo akamuuliza Mkuu wa Chuo na Majibu ya Mkuu wa Chuo alikiri kuwa Wamefunga chuo ili kujiandaa na Mitihani. Ingawa Mkuu wa Chuo alisema kuwa Mitihani ni Tarehe 10/10/2016 hivyo wamefunga kwa wiki mbili mpaka Tarehe 09/10/2016 , Mkuu wa Wilaya alibaini kudanganywa kwani ratiba ya mitihani inaonesha itaanza Jumatatu tarehe 26/9/2016.
Mkuu wa Wilaya jambo hiko likamsikitisha sana kwani ameamua Kufunga Chuo wakati wanafunzi wana Maswali yao yenye sintofahamu nyingi sana pamoja na kutaka kupewa ufafanuzi, Mkuu wa Chuo amekurupuka na kufunga Chuo Bila kuishirikisha Bodi ya Chuo. Aidha, alihoji "Mbona ni kujikanganya: inawezekana vipi ufunge Chuo bila kuahirisha mitihani ambayo tayari umetoa ratiba? Yaani mitihani itafanywa online Au vipi?"
Kutokana na Hayo DC Shekimweri amelazimika kumpumzisha Kazi Mkuu wa Chuo Kwa kumdanganya na kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutoitisha vikao vya Bodi, Kutosikiliza kero za wanachuo hata alipojulishwa Kwa maandishi na Wanafunzi hao, Kufunga Chuo Kwa dharula hali ratiba ya mitihani inaendelea na kuwashauri vibaya wanachuo kuhusu hatima yao kutokana na mkanganyiko wa mtaala.
Mkuu wa Wilaya ameelekeza Hatua zichukulie ili Mamlaka yake ya uteuzi ifuatilie na kushughulikia tuhuma dhidi yake na kuchukua hatua stahili kadiri ya Sheria.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesitisha Bodi ya Chuo na kumtaka mwenye Mamlaka na uteuzi wa Bodi aivunje Kwa kushindwa kukutana hata Mara moja Tangu Bodi iundwe Mwaka 2013 hivyo, kushindwa kutafsiri Na Kusimamia Dira kwenye Mpango Mkakati (Strategic Plan), hawana kalenda ya mwaka ya taaluma. Alihoji bila kupewa majibu ya maana uidhinishwaji wa mpango na bajeti wa Chuo unafanywa na nani iwapo Bodi haikai vikao. Alihoji, wapi vipaumbele vya Chuo, Mabadiliko na mitaala, mafanikio na changamoto za Chuo vinajadiliwa iwapo Bodi haikutani. Aidha, wanachuo hawapewi Uhuru wa kujieleza kwani hakuna uwakilishi wao kwenye Bodi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa anasema Kuhusu Changamoto za mitaala, udahili na mitihani pamoja na vyeti vya Kuhitimu tumelipokea na linafanyiwa kazi kwenye Mamlaka husika (VETA na Wizara ya Maendeleo ya Jamii).
Post a Comment