Home » » WIZARA YA AFYA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI,MAMA,WATOTO NA VIJANA

WIZARA YA AFYA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI,MAMA,WATOTO NA VIJANA

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, November 3, 2016 | 6:34 AM

WAZARA YA AFYA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI,MAMA,WATOTO NA VIJANA

Ni heshima kubwa kwa nchi yetu kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 3 wa Wafadhili wa Kimataifa wa Afya ya Mama na Mtoto (Global Financing Facility (GFF) for Every Woman, Every Child).

Wizara ya Afya tunajivunia kutengeneza na kukamilisha Mpango wa Pili wa Taifa wa Kuimarisha Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana (The National Roadmap Strategic Plan to Improve Reproductive, Maternal, Newborn and Adolescent Health in Tanzania - ONE PLAN II), ambao ndio Nyenzo ya Kutafuta Uwekezaji wa Rasilimali Fedha katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwenye eneo hili. GFF ni mojawapo ya wafadhili waliowekeza katika Mpango huu.

Hivyo jana usiku wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wajumbe wa GFF na Wawekezaji katika Afya Duniani nilitangaza rasmi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, World Bank/GFF  tutaboresha Vituo vya Afya 100 *VituovyaAfya100Kuboreshw* ili kuviwezesha kutoa huduma muhimu za uzazi na za dharura ktk Halmashauri mbalimbali nchini.

Ktk kila kituo cha Afya tutajenga Theatre, Maabara ya kuhifadhi damu, Wodi ya Wazazi na Nyumba 1 ya Mtumishi.

Vigezo vitakavyotumika kuchagua Vituo hivyo ni pamoja na;-

1. Vikwazo vya kijografia katika eneo husika mfano uwepo wa mto, mlima au barabara zisizopitika kipindi cha mvua,

ii. Idadi ya wa wananchi ktk eneo husika.

iii. Muda wa kusafiri (masaa) hadi Kituo cha Afya au Hospitali yenye Huduma za uzazi za dharura

iv. Idadi ya Zahanati zitakazotoa Rufaa kwa ajili ya huduma za dharura

v. Idadi ya Wajawazito wanaozalishwa.

Nimedhamiria tuanze utekelezaji wa Mpango huu haraka iwezekanavyo.  Kwani kukamilika kwa mpango huu itakuwa ni mchango mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ktk kuboresha Huduma za Afya hasa afya ya mama, uzazi na mtoto. Hadi sasa, ktk Vituo vya Afya 489 vya  umma ni takribani vituo 113 tu ndio vinatoa huduma muhimu za uzazi na za dharura zinazokidhi viwango. (Basic Emergence Obstetric & Newborn Care (BEMONC) and Comprehensive Emergence Obstetric & Newborn Care -CEMONC).

Nikiwa na dhamana ya kuongoza Wizara ya Afya lakini pia Mwanamke na Mama huu utakuwa ni mchango wetu mkubwa katika kuboresha huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto hasa kwa wanawake wenzangu waliopo katika maeneo magumu kufikika.

Kwa niaba ya Serikali, Wizara ya Afya na Wanawake wa Tanzania tunawashukuru sana World Bank/GFF pamoja na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation, Canada, DFID, JICA, Norway na USAID kwa kufanikisha hili.

Kwa Pamoja Tunaweza Kupunguza Vifo vya Wanawake Wajawazito nchini. *Tushirikiane*!

Ummy Mwalimu, MP.
WAMJW
Dar es salaam
3. Nov 2016

Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari
Waziri ummy akizungumza katika shughuli hiyo.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger