Home » » Ziara ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Jijini Arusha

Ziara ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Jijini Arusha

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, November 16, 2016 | 6:53 AM

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA. (CCM)

Shirikisho la vyuo vya Elimu  ya juu Taifa lilimefanya Ziara Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Ziara hiyo ililenga mambo mbalimbali pamoja na :

1.Uzinduzi wa Tawi jipya SAUT ARUSHA. Pamoja na kupokea kwa Wanachama wapya wa Tawi hilo 165.
Sambamba na IMANI KUBWA YA WASOMI KWA RAIS hatimaye  kuamua kujiunga na Chama chake Cha Mapinduzi(CCM). 

2.Hali ya kisiasa sambamba na  Utoaji wa Mikopo. Shirikisho limebaini bado changamoto zipo hasa mikoani hususani za Mikopo. Hivyo kuwaomba watumishi wa bodi ya Mikopo kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo hayo pamoja na kuwataka wakuu wa Vyuo kuhimiza Majina ya wanafunzi/Wanufaika wa Mikopo kuwasilishwa Haraka Bodi kama alivyosema Mhe Prof Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekinologia.

3.Uhai wa Shirikisho matawini na Mikoani. Shirikisho Taifa kilamewataka Wanachama kutimiza wajibu wao kama ilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha shirikisho linakuwa kimbilio la wanafunzi hasa katika Matawi katika kutatua changamoto zilizopo Mavyuoni. Hilo litaongeza Ari kwenye Matawi yetu na kuongeza Wanachama.

Shirikisho Taifa limewakumbusha Wanachama wake Wasomi kuendelea na kuongeza Nguvu katika kukisemea Chama Chao CCM, pamoja na Kazi Kubwa anayoifanya mhe Dkt John Pombe Magufuli kutekeleza AHADI na ILANI ya  CCM. Hasa Ongezeko la Mikopo ya Vyuo Vikuu sambamba na Kubaini Mikopo hewa, Elimu bora,Elimu Bure, Kubaini Wanafunzi Hewa hivyo kuokoa Fedha nyingi, Matumizi yasiyo ya lazima na Ongezeko la Mapato KODI,Uwajibikaji,Maadili ya Utumishi wa Umma,Ndege Mpya za kisasa na Kumpongeza RAIS na Serikali kwa Ujumla.

4.Uchaguzi uliopo Shirikisho na kuhamasisha makada kushiriki. Shirikisho Taifa  limetatua changamoto zilizopo Kilimanjaro hasa juu ya mkanganyiko uliokuwepo juu ya kuitangaza nafasi ya mwenyekiti Mkoa wa Kilimanjaro kuwa WAZI na Makada wajitokeze kuwania nafasi zilizopo wazi.

5.Ziara hiyo ilijikita kuelekeza kufanyika kwa Uhakiki Wanachama waliopo na kupokea Taarifa za Kiutendaji pamoja Changamoto zilizopo Mikoani pamoja na Kutoa Rai juu ya Wanachama Hewa na kuelekeza Uhakiki ufanyike kuanzia ngazi ya Matawi.

6.Shirikisho Taifa kuzindua LIBRARY MAALUM " Online library" library itakuwa BURE na itajumuisha vitabu vyote pamoja na Kiswahili. Library  itaisaidia Usomaji wa Vitabu kupitia Mtandao na itarahisisha upatikanaji wa vitabu na kuongeza Maarifa zaidi kwa Wasomi na hata Wakufunzi/Walimu. Shirikisho itazindua library hiyo hivi karibuni. Sambamba na Database yake.

Shirikisho Taifa limehamasisha  na kuwataka Wanachama walio maliza masomo kujiunga kwenye vikundi ili kujiunga na Programu ya Uzalendo "UZALENDO NI VITENDO" Ilikujitolea kufanya shughuli za kimaendeleo na kutoa mchango katika Taifa. Mfano Ujenzi wa Madarasa, Matundu ya Vyoo ya Shule pamoja na Mabweni na Nyumba za Walimu.

Pamoja na kuwapongeza Viongozi wa Shirikisho wa Mikoa ya Arusha kwa kazi nzuri na Kilimanjaro kwa kujitoa na kufanya vizuri katika kufanikisha Ziara hiyo.

Imeandaliwa na kutolewa.

Mtumishi Wenu
Daniel zenda.
Kny;K/Katibu Mtendaji
Shirikisho-Taifa.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger