Home » » UFAFANUZI WA KUTUMBULIWA DKT MWELE NA KUHUSISHWA KWA WAZIRI UMMY MWALIMU.

UFAFANUZI WA KUTUMBULIWA DKT MWELE NA KUHUSISHWA KWA WAZIRI UMMY MWALIMU.

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, December 17, 2016 | 11:39 PM

UFAFANUZI WA SAKATA LA KUTUMBULIWA KWA DKT MWELE MALECELA NA WAZIRI UMMY MWALIMU KUHUSISHWA NALO.

Ndugu Zangu Ni Masaa Kadhaa yamepita Tangu Mh Rais Alipoamua Kumtumbua Aliekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya NIMR. Watu wengi wamesema maneno mengi kwa hisia nyingi, nakwakutumia Sababu zao Nyingi pia kulingana na vyanzo vyao vingi vya Habari juu ya sakata hili.

Watanzania nivema tukatuliza Munkali kila linapotokea jambo. Na Vema zaidi tukaamua Kuishi Maisha ya uhalisia na kuacha kuishi maisha ya Matukio.

Utaratibu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) wa Kutoa Taarifa za Magonjwa ya KULIPUKA utaratibu nikwamba! Tatizo linapotokea Nchini Taarifa Hupelekwa Wizara ya Afya, Wizara hujiridhisha na Taarifa hizo, Kisha Wizara hutoa Taarifa katika Shirika la Afya Duniani (WHO) Kisha nao WHO Mpaka Wajilidhishe Ndio Directer General wa WHO anatoa Taarifa kwa Dunia kuwa Nchini Tanzania au Nchi Fulani kuna Gonjwa Fulani la Mlipuko.

Sasa Dada Yangu Dkt Mwele Alifanya Utafiti Yeye Mwenyewe na Taasisi yake ya NIMR Nakutoa Taarifa yeye Mwenyewe Bila hata Kuishirikisha Wizara ya Afya ambapo ndio Boss Wake.

Manake NIMR Iko Chini ya Wizara ya Afya inapaswa kutoa Taarifa zake Wizarani kabla haijapeleka kwa vyombo vya habari hasa jambo Nyeti kama hilo.

Watanzania wenzangu Tufahamu Kuwa Kila Kazi ina Mipaka yake.

Damage ya Dadangu Dkt Mwele Malecela kutangaza uwepo wa Ugonjwa imekuwa kubwa Sana, Mpaka imepelekea CDC/ Wamarekani kutoa hiyo alert ya ZIKA Nchini. Hii ni baada ya Tamko la juzi la Taasisi NIMR.
Tunaweza Shabikia kusema maneno mengi nakuona kama Dkr Mwele hajatendewa Haki na Mh Rais Kumtoa katika Nafasi yake, lakini Hiyo nikwasababu wengi walalamikaji Hawajui Athali za Kusema ama Kutoa Taarifa zisizo na Ukweli kwa Taifa Letu.

Lakini Pia Taarifa Ya NIMR Haikufuata Utaratibu Wa Kiutendaji baina ya Wizara na Taasisi hiyo, Kama Utaratibu ungelifuatwa basi Tusingefikia huko, Kwani kabla yakuita Waandishi wa Habari Wizara ingejilidhisha na isingetoa Taarifa kabla haijatoa Taarifa WHO kwani ndio Utaratibu wa Kutoa Taarifa kwa Umma ama kwa Dunia kwa Magonjwa haya ya Milipuko.

Mh. Rais ameamua kumpumzisha Dkt. Mwele Malecela kwa kutumia Sifa na Sababu zake yeye kwa kutumia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama nk...

Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu aliwajibika kama waziri kwa nafasi yake kwa kutoa ufafanuzi na taarifa yakiwizara kutokana na uhalisia wa taarifa za Mfumuko wa Magonjwa Nchini.
Na ilikuwa niwajibu wake kama Waziri kufafanua Jambo lile baada yakuwa tayali limekuwa halina Ukweli. Ivo Si Vizuri Kumuhusisha Waziri wa Afya na Maamuzi ya Mh Rais kwani Rais ni Taasisi na Anafanya kazi kwa Umakini Mkubwa na sio kufanya kazi kwa Mihemko nakutaka kuwafurahisha Mawaziri wake.

Waziri wa afya Mh Ummy Mwalimu kusema kuwa ndie aliemponza Dkt Mwele ama kumchongea kwa Rais kama baadhi ya watu walivyoanza kusema huko mitandaoni mimi nasema Waziri Alitimiza wajibu wake kama Waziri wa Afya, Na Mh Rais Kaifanya kazi yake yakumuwajibisha Mtumishi wake kama Rais.

Tukumbuke zama hizi ni zama za Hapa Kazi tu! na sio Mchezo mchezo na Porojo.

Niwatakie Wakati Mwema.

          Ni Mimi
     Peter L. Dafi
Mtetezi wa Wanyonge.

       0713302823

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger