Home » » WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO.

WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO.

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, May 4, 2017 | 8:40 AM

WASAFIRI WATAHADHARISHWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO.

Na.Catherine Sungura, WAMJW
Dodoma
Watanzania hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vyeti vipya
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa
Waziri Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano
Aidha amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako
Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa rai kwa  wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika tena.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger