Test Footer
UVCCM CHAMWINO YAWATUNUKU VYETI WASICHANA WALIOPATA DARAJA LA KWANZA KIDATO CHA PILI NA KIDATO CHA NNE.
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, March 15, 2021 | 9:14 AM
Chamwino:
Katibu Peter Dafi akimkabidhi Binti alieshinda Daraja la kwanza kwenye Mtihani wa kidato cha Pili
Wanafunzi wakiimba Wimbo wa Tanzania nakupenda
Katibu Peter Dafi akiingia ukumbini akiwa ameambatana na walimu
WARAKA No. 2 WA MHE. SPIKA KUHUSU UGONJWA WA CORONA
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, March 17, 2020 | 1:33 AM
Peter Msigwa alipiwa na Rais Magufuli.
Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, March 12, 2020 | 5:35 AM
UVCCM CHAMWINO WAJAZA FOMU KWA NIABA YA BARAZA LA WADHAMINI
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, March 9, 2020 | 2:56 AM
MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, July 10, 2018 | 7:08 AM
*MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATIKA JIMBO LA DODOMA MJINI*
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* leo amepokea mifuko ya Saruji 724 yenye thamani ya *Tsh 10,000,000* kutoka *Benki ya CRDB* kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji,Mkurugenzi CRDB Tawi la Dodoma *Bi Rehema Hamis* amesema kwamba Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya *Mh Rais Dr John Pombe Magufuli* na uchapakazi wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde katika kuboresha miundombinu ya Elimu.
Akipokea mifuko hiyo ya saruji,Mbunge Mavunde ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao utalenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa 1035 katika Jimbo la Dodoma Mjini ambapo kwa hivi sasa anaendesha kampeni maalum ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na kwa kuanzia mfuko wa Jimbo umetoa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 2,560 kwa kata mbalimbali.
TANZIA: Mwanajeshi wa Tanzania auawa na wengine watano hali ni mbaya
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, June 6, 2018 | 3:31 AM
MAVUNDE AWATAKA WADAU WA MICHEZO DODOMA KUSHIRIKIANA KURUDISHA HESHIMA YA DODOMA KATIKA MPIRA WA MIGUU
Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, June 3, 2018 | 11:18 PM
*MAVUNDE AWATAKA WADAU WA MICHEZO DODOMA KUSHIRIKIANA KURUDISHA HESHIMA YA DODOMA KATIKA MPIRA WA MIGUU*
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka wadau wa Mpira wa Miguu katika mkoa wa Dodoma kushirikiana na kuweka nguvu ya pamoja ili kurudisha heshima ya Mkoa wa Dodoma katika mpira wa Miguu nchini kwa kuwa na Timu ya Ligi kuu na kuongeza hamasa kupitia mashindano ya ligi mbalimbali ili kuibua vipaji.
Mavunde ameyasema hayo leo katika kijiji cha Msanga,Wilaya cha Chamwino -Dodoma wakati akifungua mashindano ya Kombe la *Kisalazo 2018* ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ndg Juma Kisalazo na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa Mh Joel Makanyaga Mwaka.