Home » , » Mbunge matatani kwa uchochezi Kenya

Mbunge matatani kwa uchochezi Kenya

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, October 18, 2012 | 9:51 AM


Sheikh Mohammad Dor
Kiongozi moja mkuu wa kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni mbunge mteule ameshtakiwa kwa kuchochea ghasia.
Mbunge Sheikh Mohammad Dor alisema kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani.
Sheikh Dor alikamatwa jana jioni baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza kufadhili vuguvugu hilo, ingawa aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka ya uchochezi.
Wanachama wa MRC wanaotaka kujitenga na Kenya
Kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe kumi na tatu mwezi Novemba.
Sheikh Dor ambaye amelaani msako unaoendelea wa polisi dhidi ya kundi hilo mjini Mombasa, alisema kuwa kundi hilo ambalo mahakama ilisema kuwa sio haramu, kwa mtu kuamua kulifadhili sio kosa.
Dor ni mmoja wa wabunge kumi na wawili wa Kenya ambao hawakuchaguliwa ingawa waliteuliwa kuwakilisha maswala kadhaa bungeni.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger