Home » » *MTOTO WA DKT. SALMIN, AMIN SALMIN AMKANA 'NDUGU JAMBAZI' KASSIM RAMADHAN JUMA (27

*MTOTO WA DKT. SALMIN, AMIN SALMIN AMKANA 'NDUGU JAMBAZI' KASSIM RAMADHAN JUMA (27

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, December 20, 2012 | 5:51 AM

Amin Salmin

*Adai si ndugu yao na hapaswi kutumia jina la Baba yake
MTOTO wa pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amin Salmin, ameibuka na kukanusha vikali kuwa 'Ndugu Jambazi' Kassim Ramadhan Juma (27) aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kukamatwa kwa ujambazi kuwa si ndugu yao katika familia.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.peterdafi.blogspot.com, Amin, alisema kuwa amesikitishwa sana na kijana huyo aliyeripotiwa katika vyombo vya habari kwa tukio la ujambazi kwa kutumia vibaya jina la Baba yake wakati si mtoto wa baba yake na wala hakuzaliwa na Baba yake na pia na ndiyo maana anaita Ramadhan Juma.
Aidha Amin alisema kuwa wakati mama yake na mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Salma Kasu, alipokuwa akiolewa na Baba yake mwaka 1990, tayari mtoto huyo Kassim Ramadhan Juma, alikuwepo na alikuwa ana umri wa miaka, 22 ambapo hadi leo ana umri wa miaka 27.
''Wakati Baba yangu akimuoa Mama yake na Ramadhan huyu kijana alikuwa na miaka 22, inamaana Baba yangu alimkuta mama yake akiwa tayari na mtoto mkubwa tu, ambaye Mama yake alizaa na mume mwingine kabla ya kuolewa na baba yangu,. sasa iweje leo ajiite mtoto wa Salmin tena katika mambo yake mabaya yasiyofaa katika Jamii, si kutaka kumchafua tu Mzee wa watu na kumpa mipresha ya bure, baba yangu''?. alihoji Amin.
Kwa kubainisha usemi wake Amin, aliongeza kuwa anawatambua vilivyo nduguze watatu, aliowataja kwa majina, kuwa ni Abal, Hamoud na Salama, ambao wamezaliwa na mama wa Kassim Ramadhan Juma, na Baba yake mzazi Dkt. Salmin Amour.
''Mimi nawatambua ndugu zangu ambao Baba yangu amezaa na Mama wa Kassim Ramadhan Juma, Salma Kasu, lakini huyu 'ndugu Jambazi' wala simtambui katika familia yetu, na wala hajawahi kutokea kati yetu kutumia jina la baba kwa 'Ujina na upuuzi' kama anavyofanya huyo ndugu Jambazi, Namuomba sana huyo Kassim Ramadhan Juma, na wenzake wasiendelee kutumia jina la Baba yangu kwa maovu yao kwani ni kutaka kumchafua tu baba yangu ambaye haitaji kuwa na presha za namna hiyo kwa sasa''. alisema Amin 
 
Habari Na Sufiani 
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger