Home » » Raia wa Ufaransa atekwa nyara Nigeria

Raia wa Ufaransa atekwa nyara Nigeria

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, December 20, 2012 | 6:33 AM

Kundi la watu wapataoo 30 waliokuwa wamejihami kwa bunduki wametumia baruti kushambulia jengo moja lenye ulinzi mkali, Kaskazini mwa Nigeria, na kumteka nyara mhandisi mmoja raia wa Ufaransa.
Idara ya polisi nchini Nigeria imethibitisha tukio hilo na kusema kuwa watu wawili waliuawa katika shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Katsina.
Mkuu wa polisi katika eneo hilo Abdullahi Magaji, amesema kundi hilo kisha likavamia kituo kimoja cha polisi, ili kuzuia maafisa wa polisi kuwafuata
Jimbo la Katsina limekuwa tulivu na halijaathirika na machafuko yanayoendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa Nigeria yanayosababishwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.



Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger