Home »
kitaifa
,
siasa
» Ni Lazima Rais JK Kikwete asaini mswada wa Katiba Mpya....!!
Ni Lazima Rais JK Kikwete asaini mswada wa Katiba Mpya....!!
Tangu Rais JAKAYA KIKWETE aanze kuwa rais wa nchi hii amepitia
kipindi kigumu sana cha uongozi kutokana na chokochoko toka kwa makundi
mablimbali ambayo mengi yalijificha kwenye migongo ya makundi mengine
kwa kuwa hayakuwa na mamlaka kumtuhumu waziwazi Rais wa nchi. Makungi
kama Jukwaa la Katiba, Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP), kituo cha
Sheria na haki za binadamu(LHRC), Chama cha wanawake wanasheria
Tanzania(TAWLA) na NGO nyingine kama hizo kwa mujibu ya malengo ya
kuwanzishwa kwazo hazikuwa na mamlaka yoyote kisheria kupiga propaganda
kumsakama Raiswa nchi kwa vile Rais anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba
ya nchi na yote aliyoyafanya amefanya hivyo kwa mujibu wa sheria na
taratibu za nchi. Jambo la ajabu ni kwamba taasisi hizo zilitumia
taasisi zingine na hasa vyama vya siasa kumshambulia Rais kwa hoja
ambazo hazikuwa na nguvu, mbaya kabisa ni pale wanasiasa walidiriki hata
kutumia maneno ambayo kwa mujibu wa kATIBA yetu walivunja sheria ya
kumtukana Rais wa nchi. Lawama kama "RAIS AMESHINDWA KUWASHUGHULIKIA
WAHALIFU" , Maneno kama "RAIS NI DHAIFU" "NCHI HAITATAWALIKA", zote hizi
zimekuwa ni hoja ambazo hazina nguvu na uvunjifu wa sheria kwa vile
sote tunatambua kuwa nchi yetu inaongozwa kwa kufuata utawala wa sheria.
Lakini Watanzania wengi wamekuwa wkijiuliza ni nini hasa kinachopelekea
baadhi ya vyama vya siasa, Taasisi zisizo za kiserikali , makundi fulani
fulani nchni kuwa na tabia hii ya kutoheshimu Serikali na kuizushia
mambo, kuchochea vurugu na hata kutoa matamshi yenye kuhatarisha amani
ya nchi yetu.
Mchakato wa Katiba Mpya umekuja kuwafungua macho watanzania kuwa kumbe,
hizi taasisi ambazo zimekuwa zikiwatumia viongozi wa vyama vya siasa
kuwapotosha watanzania, kuchochea vurugu na hata kuwa na ujasiri wa
kutoa matamko ambayo yanaweza kuhatarisha amani zote kwa pamoja,
zinapata pesa kutoka maeneo yanayofanana ndani na nje ya nchi.
Itakumbukwa kuwa, hivi majuzi Wabunge wa Upinzani waliingizwa mkenge na
chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo (CHADEMA) kususia mswada wa sheria ya
Marekebisho ya bunge la Katiba, hoja zao za msingi zikiwa ni mbili
ambazo ni kutokubaliana Rais kuteua wajumbe 166 wa bunge la Katiba na
Wazanzibari kutoshirikishwa katika maoni ya RASIMU ya Katiba mpya, hoja
ambazo hata hivyo zilionekana ni za uongo baada mawaziri wanaohusika na
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya sheria kujibu madai hayo.
Binafsi nilitegemea hoja ya wazanzibari hawakuhusishwa kwenye kutoa
maoni ingepewa uzito kwa vitendo kwa kuanzia mikutano yao Zanzibar na
ziyo bara.
Mpango huu wa CHADEMA kuwashawishi wapinzani waungane katika kususia
mswada huu, unaibua hisia ni jinsi gani NGOs kama TAWLA, GDSS, LHRC,
TGNP na nyinginezo zilivyokuwa zinajificha kwenye mgongo wa CHADEMA
kuhakikisha mchakato mzima wa kupatikana kwa Katiba mpya unavurugika.
Matukio haya yanadhihirisha wazi kuwa kuna makundi yalijipanga na kuna
makundi yameingizwa mkenge kwenye muungano wa huu ambao sasa
tunashindwa tuupe jina gani, muungano wa Wapinzani au muungano wa
CHADEMA, CUF, NCCR, TGNP, LHRC, GDSS, TAWLA ambapo leo wamekutana
viwanja vya Ofizi za TGNP, Mabibo:
1. Alianza TINDU LISSU kukiita chama cha CUF kuwa ni cha Wazanzibari;
2. CHADEMA wakaja na hoja kuwa ZANZIBAR hawakushirikishwa na wakaanza
kutoka nje ya ukumbi huku wakiangalia pembeni kuona kama CUF
wanawafuata, na walipoona wameingia mkenge wakapiga makofi na kusema
wajinga ndiyo waliwao;
3. Siku moja baada ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge, Gazeti za MAWIO
likaja na kichwa cha habari kinasema "CHADEMA, CUF na NCCR wakutana ,
kuishitaki Serikali kwa Wananchi" wakati ni kila chama kilikutana peke
yake;
4. Siku iliyofuata ndipo Viongozi hao walikutana kuhalalaisha taarifa ya MAWIO;
5. Jana Tarehe 17/09/2013 muungano huu wa wapinzani wakiongozwa na
viongozi wengi wa CHADEMA wakakutana ofisi za Jukwaa la Katiba huku vyma
vya CUF na NCCR vikiongozwa na wenyeviti pekee.
6. Leo Tarehe 18/2013 wakekutana ofisi za TGNP
Ukiangalia mtiririko huo wa matukio hauoni jinsi gani ZANZIBAR inahusishwa.
MIMI NASEMA, JAKAYA KIKWETE ni lazima asaini mswada huu ili Watanzania
tujue kilichojificha nyuma ya Pazia. Tujue kama kuna watu toka nje
wanataka kulitumbukiza taifa kwenye machafuko kwa kisingizio cha Katiba
mpya, Kinga ni bora kuliko Tiba, JK katika Katiba Mpya, "ULIAMUA,
UKATHUBUTU sasa MALIZIA" watanzania wengi tuko nyuma yako.
Post a Comment