Home »
siasa
» Mikopo kwa wanavyuo wetu na Mtizamo wa UVCCM
Mikopo kwa wanavyuo wetu na Mtizamo wa UVCCM
SASA NAELEWA
MAANA
SUALA LA WANAFUNZI WA VYUO WENYE SIFA ZA KUPATA MKOPO KWA MUJIBU WA
VIGEZO VYA BODI,KUKOSA MIKOPO NI SWALA LINALOTAKA MAJIBU YA KINA
SIO LA KUKUBALI KIRAHISI TU
NA HATUWEZI KUKUBALI KIRAHISI MAANA KIFUPI CHAKE NI KUWA SERIKALI IMESHINDWA KUSOMESHA.
NIMERIDHIKA NA MAJIBU YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU BWANA PHILIPO MULUGO NA LAZIMA YAFANYIWE KAZI.
KIFUPI ANASEMA;
KWA MUJIBU WA BAJETI YA BUNGE WOTE WENYE SIFA WAMEPEWA MIKOPO BAJETI IMEISHA NA WANACHUO 2000 WENYE SIFA WAMEKOSA.
SASA WAO HAWANA CHA KUFANYA KWA MUJIBU WA TARATIBU LAZIMA WARUDI
BUNGENI KUOMBA BUNGE LITAFUTE CHANZO KINGINE CHA MAPATO ILI WALIOSALIA
WALIPIWE.
ATA KAMA NIKWAKULIPIA LINE YA SIMU 200 KILA MTU MWENYE UWEZO ALIPE TU NDUGU ZETU WASOME.
1.MASIKINI NA MAYATIMA WASIO NA UWEZO
2.WALIOCHAGUA FANI ZENYE KIPAUMBELE CHA SERIKALI
3.WALIOPATA VYUO VYA KUSOMA
HIVYO NI MIONGONI MWA VIGEZO VYA MSINGI .
SASA TUSISEME AU KUITAKA SERIKALI ILIPE TU
MIMI NAONA TUKUSANYE MAJINA YOTE YA WENYE SIFA
TUWE NA HOJA TWENDE DODOMA TUMWAMBIE WAZIRI MKUU
NA WAZIRI WA ELIMU
UVCCM INAOMBA WANAFUNZI HAO WENYE SIFA MNTAFUTE PAKUZIPATA PESA WALIPIWE.
HII NDIO KAZI KUBWA YA UMOJA WA VIJA WA CCM
NA HAKIKA INAWEZEKANA
UVCCM TUTAENDA PAMOJA DODOMA
ATA KAMA KWA MGUU.
MPAKA BODI WAONGEZEWE FEDHA NA NDUGU ZETU WENYE SIFA WASOME
HATUWEZI KUENDELEA KUWA VIJANA KAMA WA VYAMA VILE VINGINE WAKULALAMIKA TU HAIKUBALIKI.
LETENI MAJINA TUJENGE HOJA
VIONGOZI WAJUU UVCCM TUTAENDA NAO DODOMA.
TUTAFIKA NA TUTASIKILIZWA
TAYARI TUMESHAWASILIANA NA KIONGOZI WA VIJANA WALIOANDAMANA HADI WIZARANI
TUPATE DATA
TWENDENI
NA KWAMUJIBU WA NAIBU WAZIRI WANACHUO 2000 WAMEKOSA MKOPO
SASA KILA MMOJA KWA MWAKA AKIPEWA MILIONI 2 KAMA WATANZANIA CHINI YA SERIKALI TUNATAKIWA KUTAFUTA BILIONI NNE ZA ZIADA
SASA WAZIRI MKUU TUNAKUJA DODOMA BILION NNE TUTAPATEJE
JAMANI TWENDENI
Na Gladness Theonest
PHILIPO MULUGO
"Kasungura kadogo na mkumbuke kuwa mkopo ni kuomba kuna kupata na
kukosa...hivyo wale waliokosa na walikuwa na vigezo watafute watu
wengine wenye uwezo wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata watume tena
maombi," alisema.
Alisema kilio chao amekisikia na leo atazungumza
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na malalamiko yao ambapo suala
hilo litapelekwa Bungeni ili kujadiliwa.
"Kama Bunge litaamua
kupunguza fedha kutoka kwenye bajeti zingine ili kusomesha wanafunzi
hao. Bunge litaamua kwani Serikali ina nia nzuri sana kwani hadi sasa
imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu hawarudishi," alisema.
Alitaja sababu nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia
uhitaji, kwani kuna masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu
wa wataalamu.
Alitaja fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na
wahandisi. Alitaja sababu nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni
waombaji kukosea majina na vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa
kwenye vyombo vya habari warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.
Alisema waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa 6,000 lakini waliorudi
kufanya marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000 walikuwa na
vigezo lakini wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).
Wanafunzi waliokosa mikopo walisema kama wenzao wameweza kupata mikopo
kwa asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana ili wote waweze kupata
GAZETI LA MAJIRA
Na Asenga
Post a Comment