Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.
Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.
Polisi wakichunguza vidonge ambavyo huyu mrembo alikuwa amevimeza.
Waandishi wa habari wakipiga picha vidonge vya heroin alivyokamatwa navyo mremboi huyu wa Kitanzania.
![]()
Mrembo Jackie Cliff akamatwa na heroin China
Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, December 27, 2013 | 12:31 AM
Related Articles
- UVCCM CHAMWINO WAJAZA FOMU KWA NIABA YA BARAZA LA WADHAMINI
- MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK
- TANZIA: Mwanajeshi wa Tanzania auawa na wengine watano hali ni mbaya
- Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christine Mndeme , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole Sendeka.
- AJALI MBAYA YAUWA MAAFISA WA SERIKALI
- KIFO CHA AKWILINA NI MTAJI WA SIASA KWA WANASIASA UCHWALA WA TANZANIA.
Post a Comment