Home »
siasa
» Mzee Mtei Kasema Zitto HAITAJIKI CHADEMA, UAMUZI KAMATI KUU MWISHO
Mzee Mtei Kasema Zitto HAITAJIKI CHADEMA, UAMUZI KAMATI KUU MWISHO
Mtei: Zitto Hahitajiki ndani ya CHADEMA, Uamuzi wa Kamati Kuu ni wa Mwisho!
Waku, Katika pitia pitia katika magazeti ya mtandaoni, nimekutana
na kauli kutoka kwa mwasisi wa CHADEMA Mzee Edwin Mtei kwenye gazeti la
Mwananchi. Pamoja na mambo mengine, taarifa inasema
"Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake
au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.
Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais ni vizuri akatafute
vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki.
Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana shida...
“Lakini huwezi kuwapeleka viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu.
”Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali ndani ya Chadema na hata kuzua
mitafaruku ya hapa na pale huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho." Mwisho wa kunukuu.
My take: Je CHADEMA kama chama ni mali binafsi ya Mzee Mtei ama
Wananchama? Kama ni mali ya wanachama, huo ujasiri wa Mzee Mtei kudai
kwamba mwanachama fulani hatakiwi ndani ya chama anatoka wapi? Tujadili.
source: Zitto aibuka kidedea mahakamani - Kitaifa - mwananchi.co.tz
Update: Kauli nyingine iliyopatwa kutolewa na Mzee Mtei dhidi ya Mhe.
Said Arif alipojivua Umakamu mwenyekiti kwa kutuhumiwa kumsaidia Mhe.
Pinda kupita bila kupingwa uchaguzi wa 2010 na Kupinga Mzee Mtei
kumchagulia watu wa kufanya nao kazi. "Aache Kulalamikia, kwasababu
wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, mimi nilisimamia uchaguzi.
Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA
Taifa, alipaswa kujichunguza kwanza."
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Tutaendelea-kuwafukuza-wasaliti/-/1597296/2086242/-/a6i2v1z/-/index.html
Post a Comment