Home » , » MTANZANIA ALIYEWAUA KIKATILI WANAWE WAWILI HUKO AUSTRALIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

MTANZANIA ALIYEWAUA KIKATILI WANAWE WAWILI HUKO AUSTRALIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, December 21, 2014 | 3:08 AM

MTANZANIA ALIYEWAUA KIKATILI
WANAWE WAWILI HUKO AUSTRALIA
AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA!
Charles Mihayo, (36) mzaliwa wa
Tanzania ambaye mwezi April, 20, 2014
aliwauwa watoto wake wawili wadogo
wa kike nyumbani kwake huko
Melbourne, Australia amehukumiwa
kifungo cha maisha.
Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na
mke wake, hasira zilimfanya bwana
Mihayo kuamua kufanya ukatili wa
kukatisha uhai wa watoto wake
mwenyewe Savannah (4) na Indianna
(3), ili tu kumuumiza mke wake kama
njia ya kumlipizia kisasi. Inadaiwa kuwa
aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto
baada ya kucheza nao.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji
hayo yalipofanyika, mama wa watoto
hao aliwapeleka kwa baba yao bwana
Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao
aliwafanyia shopping ya nguo na viatu
vipya.
Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu
yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi
video wakicheza muziki huku akicheza
nao. Na katika video ambayo polisi
baadae waliiona, alisikika akiwaambia
binti zake wamuoneshe mama yao nguo
mpya alizowanunulia, na walifanya
hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa
mbele ya camera na kusema
“tutamuonesha mama kitu kingine
dakika kumi zijazo”, na kuendelea
kucheza nao hadi alipowakandamiza na
mto (pillow) hadi kufa.
Baada ya kufanya mauaji Mihayo
mwenyewe aliwapigia simu polisi
ambao baada ya kufika nyumbani
kwake wakiwa mlangoni aliwaambia ,
“Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto
wangu. Inabidi mumuulize huyu [mama
yao] sababu.
Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa
tayari wamefariki huku wakiwa
wamevalishwa nguo na viatu vipya
ambavyo walinunuliwa na baba yao siku
hiyo.
Licha ya kuhukumiwa kifungu cha
maisha, Charles Mihayo anatakiwa
kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla
ya kupata haki ya kupewa msamaha.

Mtanzania Aishie Australia Afungwa Maisha Baada ya Kuwauwa Wanae Wawili baada ya Kuachwa na Mama yao.

Watoto waliouwawa ndio hawa.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger