Home » » BASI LA GREEN STAR LASABABISHA AJALI KWA WAZIRI FENELLA MUKANGALA

BASI LA GREEN STAR LASABABISHA AJALI KWA WAZIRI FENELLA MUKANGALA

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, June 29, 2012 | 8:46 AM



Wazir wa habari, vijana, Utamaduni na michezo Mh DKT Fenella Mukangala, amepata ajali mbaya leo asubuhi Huko Katika kijiji cha Nyandekwa, Igunga, mkoani Tabora,
Waziri alikuwa anatoka Dodoma kwenda Jijini mwanza katika ufunguzi wa mashindano ya taifa ya michezo Vishale(darts)

Kamanda wa POLICE mkoani Tabora amethibitisha kuwa;

Waziri amepata ajali hiyo baada ya basi lenye namba za usajili T 939 TRA mali ya kampuni ya GREEN STAR,lililokuwa likiendeshwa na Daniel Chawa umri miaka 32, kuwa "imeovateki" au kulipita gari jingine katika kilima, kabla yakukimaliza kilima hicho ndipo ilipokutana na  Gari ya waziri Fenella Mukangala akitoka Dodoma, Dereva wa waziri huyo alijalibu kulikwepa Basi hilo ndipo ajali hiyo ilopotokea....!!!

Kwenye Gari ya waziri kulikuwa na watu watatu, Dereva wa gari ambae ni Saidi Komando, Makamo wa waziri Mh. Femela Mkangala na Mh DKT Fenella Mukangala, baada ya ajali hiyo walikimbizwa Hospitali ya wilayani Nzega kwa matibabu.

 Kwa sasa waziri  anaendelea vema na ametoka Hospitali yuko Forest in Hotel Nzega amepumzika na kesho atarejea Dodoma.

Dereva wa basi ameshikiliwa na Police Igunga na kesho atapandishwa kizimbani kujibu mashtaka ambayo meme na wewe Hatuyajui.
Gari ya waziri huyo yenye number STK 8780 land Cruiser Imeharibika vibaya sana, imetolewa eneo la tukio nakupelekwa kituo cha POLICE Igunga.

 Rai ya kamanda wa POLICE Tabora ameasa "Madereva kuzingatia sheria kwa wakati wote".


Nitazidi kuwaletea habari na picha za matukio zaidi watu wangu waukweli.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger